Monday, October 22, 2012

WOMEN IN BALANCE YAPATA MWITIKIO NA YAFANA SANA!!!




Kiukweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, women in balance Kitchen party gala ilinoga mno! Mi nilikuwepo, watu walifurika na kupitiliza! Na hii ni ishara nzuri kwamba mkutano huo umekua na pnahitajika juhudi za dhati tena za makusudi kuiimarisha ili kuwakomboa wanawake na wanaume katika fikra mgando zinazoyumbisha ama hata kusambaratisha ndoa zao! 



Watu wakaanza kuingia! Huyo mwenye skirt ya orange na blaizer nyeusi ni Babra Hassan wa Power Breakfast  Clouds Fm


Ukaguzi ni muhimu popote pale, basi ilibidi subra ili ukaguliwe! Na mdada white ni Mrs Urio


                        Nyomi lilikua hivi! Na huu ni upande wa kushoto wa jukwaa! Walifurika babake




                                                         Niamini kulijaa mpaka pomoni!





 
wanasaikolojia wawili! walikuwepo kama tulivyoahidiwa, Chris Mauki kutoka chuo kikuu cha Dar-es-Salaam, na Aunt Sadaka walitoa mambo mazito ambayo hapa hayatoshi kama ulikosa pole, jiwende mwakani uwepo kwa wewe wa Dar.Chris yeye alitoa tofauti kati ya mwanamke na mwanaume,jinsi Mungu alivyomuumba mwanamume,makosa ya wanawake, lakini kubwa kuliko yote ni kwamba 85 percent ya mahusiano ni tatizo mada tamu na nzuri, kwa upande wa Aunt Sadaka ye alimchambua mwanamke wa mfano anayemtamania! uuuf alitishaje?!



Aunt Sadaka akimkaribisha sextherapist Getrude Mungai kutoka Nairobi nchini Kenya, mwenye wa Mombasa na aliyeketi ni msaidizi wa Getrude, samahani sikumuuliza jina, oh.lakini Getrude aliwataka wanawake wasitumie style ya rabbit style badale yake watumie dogstyle na lazima uinue kichwa na akawataka wanawake waache kufake kwenye love! yapo mengi we ni mafunzo kwa vitendo.



  Mama Victor upande wa kidini zaidi , naye alikuwepo. kwa bahati mbaya saa nne na dk 15 wakati mama Victor alipokua anapanda mi nlikua naondoka hm kujiandaa na show ya jj 360 ya Power Breakfast inayoanza mapema sana so sikumsikiliza naomba radhi kwa hili.

Skylite band band mpya inayokuja kwa kasi na kutishia zilizokuwepo, ilikuwepo kutoa burudani! saaafiii


                                   Mary Lucas na Sonny kutoka skylite Band wako vizuri

Annette Kushaba mashalaah anajituma jukwaani kiukweli! Na Sam naye pembeni hapo kwa kuimbaaa weeeh! safii

Shamim Zeze wa 8020 Fashions naye alikuwepo kuchukua matukio! Mashallah mi hupenda anavyovaa, make up na hata hair style, na suala la mambo nloyasema Chris Mauki  kwamba wanawake hata wakiwa chooni husubiriana mmoja atoke na waulizane alikosuka ama alikoshona nguo, huko huko maliwatoni, lakini wanaume wanaweza kujipanga hata watano wakashii pamoja na asijue wa pembeni yake amevaa nini ama mr Victor wake yukoje, ye akimaliza shughuli zake anatoka safi.


mtoto mzuri huyu ni kutoka TSN supermarket wadhamini wa Kitchen Part Gala, anaitwa Lizbert ndiye meneja masoko wa kampuni hiyo! mashallah!

                         Dina Marios mama ya shughuli Big up ndiwe mwanamke wa mfano mama.
 Mc wa shughuli Gea Habib wa Leo tena, alikua busy kuhakikisha watu wake wanafika kwenye k.Gala.

ilikua utaratibu ni kukaa kwa meza ya watu kumi, na unakuta umewekewa jina lako ili usipate taabu, mwenye jina aja hapo chini.
             Mwenye miwani ndiye Rose Nyanje aliyeko kitengo cha masoko Clouds Media Group!
                            Babra Hassan na Teddy Mapunda a.k.a Aunt T naye alikuwepo safi!
         Juhaina Kussaga ambaye ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions hapa yu na nduguye.

 Mheshimiwa Sofia Kessy,japokua alikua safarini kutoka Kilimanjaro ambako ndiko alikopata nafasi wa kuongoza vijana kupitia chama cha mapinduzi, alihakikisha hakosi Kitchen Party Gala , alipendezaje!
  Clara Manyinya wa mjengoni Clouds Media Group,binti asiyekaukiwa tabasamu na aso utani na kazi yake naye alikuwepo! safi Clara hivyo hivyo muhimu kujishirikisha .

Jamani kwa leo zatosha nyingine ntawawekea kesho! asante kwa kunielewa 

No comments:

Post a Comment