Haya sasa raha jipe mwenyewe! Namna ya
kusherehekea ni wewe utakaye amua namna utakavyoa adhimisha tukio flani
maishani mwako. Kwenye burudani ndo drama zaidi kiukweli! Wao wana swagger zao
za hatari na hua kama wamekatika mshipa wa aibu hivi! Pindi wanapoamua kufanya
mambo yao!
Uwe mtoto wa mchungaji, au wa yeyote,
wakiamua wameamua na hakuna wa kuzuia hilo! Na naamini wao pia wanaamini ndo
njia ya kuwashika mashabiki wao, mfano hai ni Lady Gaga,Madonna na wengineo wan
je, na wengi huingia kwenye shows zao wakitarajia kimbwanga kipya kutokea! Hii ni
biashara ya burudani na safari hii ni mwimbaji Wyclef Jean, yeye ameamua
kutupia picha yake katika ukurasa wake wa Twitter,akionekana amejipaka mafuta
ya watoto baby oil na amesimama juu Ya pikipiki akiwa na kiwinda
tu
Kwenye ukurasa huo wa twitte
aliandika kinachosomeka 'TODAY I AM 43 YEARS OLD! I look And feel 26! U cant
keep ‡ good Man down! Keep ‡ smile when they want you to frown!' maneno ya
Wyclef ambayo sikutaka kuyazimua! Nimekupa makavu kama yalivyo.Wyclef alikua ni
mmoja kati ya wanamuziki walokua wanaunda kundi la The Fugees lililovunjika mnamo mwaka 1997,na kuamua
kufanya kazi zake kivyake!.
Albam yake mpya ilikua itoke mnamo
mwaka wa jana 2011 lakini bado ameiminya kwasababu zake , pengine imesababishwa
nay eye alipojaribu kuwania nafasi ya juu ya uongozi kama Rais huko Haiti mnamo
mwaka 2010 ingawa hakushinda katika uchaguzi huo.
Siku za karibuni Jean alimake headlines pale alipofunguka kwa aliyekua mzazi mwenziwe Lauryn Hill kua alimdanganya
kua ndiye baba halisi wa mtoto wake wa kwanza wa kiume kumbe sibvyo! Mwana hip
hop huyo alikua na mahusiano na mwimbaji huyo wakati kundi lao lilipokua katika
uhai na kutamba sana miaka ya tisini ulimwenguni na kwasababu Jean alidanganywa ikawa ndo chanzo cha
kuachana kwao na ukweli ni kwamba mtoto ni
mjukuu wa Bob Marley baba akiwa ni Rohan ingawa mwenyewe anakana.
Rohan alikua kwenye mahusiano na Hill kuanzia mwaka 1996 hadi 2004,ameliambia jarida la TMZ alikubali kua mtoto huyo ni wake pindi
alipojua [Lauryn] yu mjamzito
Rohan, amezaa watoto watano na mwimbaji huyo kabla hawajaachana na
alidhani rapper huyo anatafuta kuuza kitabu chake kwa kumpakazia mambo na hana
muda wa kuyajibu hayo ayasemayo na anajua kua anajichanganya mwenyewe.
Hata hivyo mwandishi huyo wa nyimbo
kutoka Haitian, bado anaishi na mkewe Marie Claudinette kwa miaka 18 sasa! Amesimamia
story yake.Anakataa kua hakukua na namna ya yeye kuwepo hospitalini kumpokea
mtoto asiye wake na hakukua na muda huo, lengo ni kusema ukweli, ni wazi ukweli
unauma lakini uongo unauma zaidi.
Japokua ni heka heka za kuzaliwa kwa Jean bado maneno ya
kutupia hayajakata! Sijui kikomo chake ni lini?
No comments:
Post a Comment