·
Ni ushirikiano kati ya Vodacom na Heritage Tanzania
kuzindua bima ya Faraja, Bima ya mazishi na ajali.Wateja kununua na kulipia Bima kupitia M-Pesa.
·
·
Huduma ya bure kutolewa kwa wateja watakaolipia huduma
mara kumi kwa Mwezi.
Dar-es salaam, Octoba 3, 2012
… Huduma ya Vodacom ya M-Pesa
imezidi kupiga hatua baada ya kuwawezesha Watanzania kufanya malipo yao ya bima
kupitia huduma hiyo.
Hii inafuatia ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania na Heritage Tanzania
kuzindua Bima ya Faraja, ambayo ni Bima ya mazishi ambayo inamuwezesha mlengwa
kulipwa fedha taslim za mazishi kwa muhusika mwenye bima. Bidhaa mbalimbali
ziko katika mpango huo ili kukidhi mahitaji ya wateja na bajeti ya malipo ya
kila mwezi kuanzia shilingi 20000/= fadi 9800/= kwa Mwezi.
Mteja ana chaguo la kuongeza malipo kwa kuongeza huduma ya vifo
vinavyotokana na ajali kulingana na faida na sera zao. Ongezeko hili la ziada
litaongeza kiasi cha faida mara tatu kwa ongezeko dogo la malipo.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema wateja wa Vodacom
wanaotumia M-Pesa, wataweza kujipatia bima ya bure kwa mwezi.
“Wateja wetu wote ambao watafanikiwa kutuma pesa walau mara 10 kwa Mwezi
watapata bima ya bure ya kiasi cha
Shilingi laki mbili kwa mwezi unaofuata,” amesema Meza.
Suala la kipekee katika huduma hii ni kwamba hakuna haja ya kujaza fomu ili
kujiunga na bima hii. Mteja atajiunga kwa njia rahisi kwa kupiga *150*00# na
kuchagua kipengele cha bima. Vodacom inahakikisha kuwa wateja wote wa M-pesa
wanaweza kupata huduma hii ili kuwa na amani ndani ya familia zao.
“Ni muhimu kuthibitisha kuwa taarifa
zako ni sahihi, na kuthibitisha kuwa unaelewa vigezo na masharti. Taarifa zako
zitatumwa moja kwa moja kwenda Heritage Tanzania,” alisema Meza na kuongeza
kuwa, “Unaweza kuchagua aina ya bima ambayo inakidhi mahitaji na bajeti yako,”
Bima hii ya Faraja
pia itawawezesha kila mmoja kubadili au kuongeza kiwango chake kwa ile yenye
faida zaidi kulingana na mahitaji yao na mabadiliko ya bajeti katika maisha
yao.
Kwa taarifa zaidi
kuhusiana na huduma mteja atapiga 0764 300001 bure au vipeperushi kutoka kwa
wakala wa M-Pesa nchini.
Mwisho
… ///
No comments:
Post a Comment