Wednesday, October 24, 2012

KITCHEN PARTY GALLA PART II

juzi niliahidi kukuletea hizi picha zilizosalia, lakini naomba radhi jana nlitingwa mno, so kiduchuu zilizobaki hizi hapa.Huyu ni Chriss Mauki mwanasaikolojia anayechukua masters yake South AFrica juu ya mahusiano, na usione karatasi alizoshika ndogoooo, ukadhani hamna kitu! eh umesahau kua hamna hamna ndimo mliwamo? alitisha kiukweli i wish kama wanaume wangekuwepo ili nao wamsikie Chris maana alikua anatoa vitu halisi katika maisha ya kila siku. wow! congrats brother.
Getrude Mungai na Chris walikua kama watani wa jadi siku hiyo! na haya mazoezi ilikua ni katika harakati za kuwafanya wanawake wawavutie wenza wao , na practice make it !? PERFECT sio? eeeh ndo maana yake.tulifanya mazoezi mengi na kushare mengi kati ya Mambasa ya Mambasa na Bongo! chezea mapenzi weye? utalia kilio cha mbwa mdomo juu oh! shaurilo kaza buti, simamia mwanangu ahahahaha.
Getrude Mungai sexology, ana ngozi nzuri na ni mzuri pia, lakini pengine mbali ya kula,kulala pazuri,nguo bora, wataalamu wa mambo ya mapenzi wanasema kua usipofanya sex vya kutosha unakua na msongo,mgomgo kuuma,kichwa kuuma na ngozi husinyaa, lakini ukiipata kwa wakati na ukatosheka abhaaaaas! utakua nyororoooooooo!


vifalio kama hivi vilivyoletwa na bi Getrude vilihamasishwa kutumika wakati wa chakula cha usiku kwa wakubwa tu! na yeye alitwambia ana kijitray chumbani kwake kilichofurika vikorombwezo vya kuchokolea pweza mwambani na mashallah kufanikiwa mno, ikiwemo kumfanyia vituko laazizi wake kwenye mtoko wa jioni na laazizi anapotaka kuhakiki anakuta kweli! anapagawaje? hahaha asante mama

hiki kazi yake inajieleza! nachelea kua mchimvi weee! hhaha soma mtafute Dina Marios maana kuna vingine kaachiwa auze we muulize tu.

Picha nzuri watazipata kina Michuzi na akina Muhidini Maphoto lakini hata mimi naweza! nimejaribu na taswira ya ubapa ya akinamama walopata mzuka wa Skylite Band wakiserebuka, walau umeoneeee eh! samahani kwa picha hii ya ubapa hahaha lol.



 Shamim aka Zeze na inginia jiji amah haha Gea Habibu MC wa siku hiyo! wamependezaje? mwanamke mvuto babu eh! ndeiyo! inaongeza mahaba na mume ama bwana kama waitavyo Mambasa bwana hachoki kukutazama. upo we haya wee jiache rafu uone kitakachotokea usije mlaumu mtu mi nakwambia hivyo, uwe mwanamke ama mwanaume!

Basi sawa! muandaaji na alosababisha East Africa na zaidi sana  wanawake  wa Bongo ambao wanaokisiwa kukaribia kufikia 1000, kukutana pamoja Dina Marios aka SuperMarios, anaonekana akiwa amevunja pozi na mgeni wake, wote wanavutia watoto wa East Africa hatuzuriani yakhee.
nywele pale kati upo?
Kwenye kitchen Party Galla moja ya vitu ambavyo nilazima ukutane navyo ni styles za nywele! wee wanawake waliripukaje? nguo ndo usiombee, make up je weee acha kabisa! mi nlichopenda kwa huyu dada ni naturality yake bhaaaas, tazama ngozi, nywele ni style ya dread kikubwa zaidi ni shingo yake na enzi za mababu na bibi zetu shingo kama hii iliitwa SHINGO YA UPANGA, AMA MATWIGA ah mashalaaah.
Joyce Shebbe mkuu wa chumba chetu cha habari naye aliondoka na style ya dread kiukweli zilipendeza mno  na ngozi yake nayo imetulia!alisukwa kwa ustadi mkubwa na bibi huyu hakosi katika Kitchen Party Galla yupo kila wakati na hushiriki mzima mzima! asante, hahaahahahah
                   Nnapozungumzia styles mcheki mdada hapo kati mashallah.



Betty Florist kutoka namnanga naye alikuwepo


Cynthia Henjewele Mc na Florist mahiri hapa Dar mke wa Mc Henjewele My brother naye alikuwepo amenonaje? asante kaka kwa kumtunza wifi! ndeiyo.samahani lakini mwanga sikuulenga ukaingilia picha uwii ntaweza tu.


Warembo wanaofanya kazi hapa Tanzania, jirani zetu kutoka Kenya walikua na table yao mwenyeji akiwa ni Rose Nyanje.
Msosi wenye ladha maridhawa kwenye shughuli hii ni muhimu, na huwa ni mtamu, tena kila wakati ubunifu huzingatiwa! ndeiyo!
INATOSHA JAMANI MPAKA WAKATI MWINGINE MARA NYINGINE, KUTOKA DIAMOND VIP HALL NI MIMI MWENYEWE. HAHAH LOL.

No comments:

Post a Comment