Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA
Tanzania,Aldo Mfinde wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar tayari kwa Uzinduzi rasmi wa maonyesho ya VICOBA Tanzania.Wa pili
Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga na Kulia ni
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.
Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo
Mfinde akizungumza machache wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka
Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa VICOBA
uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.wa Tatu kulia
ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh. Edward Lowassa.Wengine ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh.
Makongoro Mahanga (pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa
Simba.
Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akimpongeza Mratibu wa
Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde mara baada ya kumaliza kuitambulisha
Kamati ya VICOBA Tanzania iliokuwepo viwanjani hapo.
Burudani ya Ngoma za
Asili.
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania,Bi. Magreth Mapunda akisoma Risala
ya Chama chao hicho mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa wakati wa hafla ya
Uzinduzi rasmi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo na
Wajasiliamali wa VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania,Bi. Magreth Mapunda (kushoto)
akikabidhi Risala hiyo kwa Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba akisalimia Wanachama
wa VICOBA Tanzania.
Naibu Waziri wa
Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha
Mgeni Rasmi kuzungumza na Wanachama wa VICOBA
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akitoa hotuba yake mbele ya wanachama wa VICOBA Tanzania wakati hafla ya
Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na
Wajasiliamali wa VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam.Katika Hobuba yake,Mh. Lowassa aliwapongeza wana VICOBA
kwa kuweza kujiajiri,kwani tatizo la ajira nchini bado ni tatizo kubwa na ni
bomu linaweza kulipuka wakati wowote.Maonyesho hayo yataendelea mpaka jumamosi
ijayo Oktoba 27.
Waziri Mkuu Mstaafu
na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akiteta jambo na
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga
akajichanganya na kujiachia! weweee
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akibonyeza kitufe kwenye kompyuta ikiwa ni ishara ya Uzinduzi rasmi wa
Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali
wa VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akiwapungia mkono Wanachama wa VICOBA wakati wa kuwaaga mara baada ya kufanya uzinduzi
wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali
wa VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu
na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na baadhi ya Wanachama
wa VICOBA mara baada ya uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara
ndogo ndogo na Wajasilia mali wa VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu
na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na Naibu Waziri wa
Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga
Baada ya mgeni kuondoka, burudani iliendelea.
No comments:
Post a Comment