Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akielezea jinsi shirika
hilo linavyoshirikiana na serikali ya Tanzania katika kufanikisha miradi mbali
mbali ya maendeleo katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kwenye kukuza uchumi.
Umoja wa Mataifa umeanza kuadhimisha wiki
mahsusi kwa ajili ya Umoja huo kwa kufanya shughuli mbalimbali ambapo nchini
Tanzania taasisi za Umoja wa Mataifa, Serikali ya Tanzania na mashirika ya
kiraia wanakutana kuzungumzia maswala mbalimbali yahusuyo maendeleo, utawala
bora na njia za kupiga vita umaskini uliokithiri.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa shirika la Umoja
wa Mataifa linalohusika na Maendeleo nchini Tanzania UNDP Philippe Poinsot,
amesema Tanzania ni nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo inawajibika
vizuri kwenye umoja huo.
Mbali na hayo Mkurugenzi huyo wa UNDP amesema
kuwa Umoja wa Mataifa unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza umasikini
uliokithiri nchini Tanzania ambapo takriban dola za Marekani lakini nne milioni
hutolewa katika kipindi cha miaka minne.
Wiki ya umoja wa mataifa imeanza kuadhishwa
Oktoba 17 na itafikia kilele Oktoba 24 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment