Wednesday, October 17, 2012

MAKAMU WA RAIS AOMBOLEZA KIFO CHA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo  ya msiba wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Ukonga jijini Dar es Salaam, kushiriki katika shughuli  za msiba huo na kutoa heshima za mwisho.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Ukonga jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, marehemu,  Liberatus Barlow.


No comments:

Post a Comment