Thursday, October 25, 2012

MAADHIMISHO YA MIAKA 67 YA UN DAR-ES-SALAAM


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta  akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za  maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa katika viwanja vya Karimjee  jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesisitiza juu ya umuhimu wa nchi za bara la Afrika kutathmini na kupima mafanikio ya malengo 8 ya millennia pamoja na kuongeza juhudi katika kupambana na umasikini na janga la njaa.


 Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou akitoa salaam za Umoja wa mataifa wakati wa maadhimisho ya 67 ya Umoja huo jijini Dar es salaam.



Baadhi ya wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania  yaliyoongozwa na kauli mbiu ya uboreshaji wa maisha ya watu na uhifadhi endelevu wa mazingira kwa maisha bora  jijini Dar es salaam

Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium Schools) ambao walikuwa kivutio wakati wa maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakiwa katika gwaride maalum kupamba sherehe hiyo

Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium Schools) wakiimba wimbo maalum uliobeba ujumbe wa kuhimiza utunzaji wa amani miongoni mwa mataifa wakati wa  maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania  jijini Dar es salaam.


Wanafunzi wa shule ya sekondari Azania wakiimba wimbo uliobeba historia na mafanikio ya Umoja wa mataifa tangu kuanzishwa kwake  jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kupokea maelezo ya awali kutoka kwa Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Hoyce Temu (kulia) kuhusu mabanda ya maonyesho yaliyoandaliwa rasmi kuonyesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na umoja wa mataifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini Tanzania

Wadau wa kuhifadhi mazingira wakionyesha  baiskeli za miguu miwili zisizotumia mafuta ambazo  ni rafiki wa mazingira zenye  uwezo wa kusafiri kutoka eneo moja hadi jingine wakati wa maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment