Rwanda imechaguliwa kuwa mwanachama
wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa miaka miwili ijayoKura hiyo
inakuja siku moja baada ya ripoti ya Umoja wa mataifa kufichuliwa ikisema kuwa
nchi hiyo inaunga mkono waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Nchi
zitakazoshikilia nafasi tano zisizo za kudumu katika baraza hilo lenye
wanachama kumi na tano, ziliamuliwa na umoja wa mataifa jana.Argentina, Australia, Korea Kusini
na Luxembourg pia wameteuliwa kuketi kwenye baraza hilo.Kulingana na ripoti hiyo ya
wataalamu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa na ambayo ilifichuliwa na
shirika la habari la Reuters, waziri wa ulinzi wa Rwanda anaongoza kw akutoa
amri kwa waasi wa M23 wanaoendeleza uasi Mashariki mwa DRC tangu mwezi Aprili.Wataalamu pia walishutumu Uganda kwa
kuunga mkono waasi.Rwanda na Uganda, zimekanusha madai hayo.
Rwanda imetuhumia kuunga mkono waasi
wa M23 Mashariki mwa Congo.DRC ilielezea upinzani kuhusu Rwanda kugombea nafasi
hiyo lakini mmoja wa wanadiplomasia wa Rwanda alisema kuwa wapiga kura
wasingeshawishiwa na ripoti hiyo isiyo na msingiRwanda itachukua nafasi hiyo
ambayo inashikiliwa na Afrika Kusini mwezi Januari mwakani.
Katika taarifa ya waziri wa mambo ya
nje Rwanda, Louise Mushikiwabo serikali yake inaweza kutoa mwongozo kuhusu
mambo yanayohusiana na vita na amani kwa sababu ya mauaji ya kimbari
yaliyotokea nchini humo ambapo watutsi milini moja waliuawa.
No comments:
Post a Comment