Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed
Gharib Bilal akiwa na Rais mpya wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya rais mpya wa Malawi kukabidhiwa madaraka leo
jijini Brantyre kwenye hoteli Sunbird. Baada ya kukutana viongozi hao walipata
fursa ya kuzungumzia masuala la kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili na
kukubaliana kuendelea kuwa na mahusiano mema kama nchi zinazoishi ndugu na
jirani. Picha kwa Hisani ya Ikulu ya Malawi
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI SHEREHE ZA
MAKABIDHIANO YA URAIS NCHINI MALAWI
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DkT. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatatu
Juni 02, 2014 ameshiriki katika sherehe za kukabidhi madaraka kwa Rais mpya wa
Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika katika sherehe zilizofanyika kwenye
uwanja wa Kamuzu Banda jijini Blantyre. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais
wa Botswana sambamba na wawakilishi wa nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika
Kusini na nyinginezo.
Akihutubia
baada ya kukabidhiwa sime ambayo ni ishara ya kuwa kiongozi wa watu wa Malawi,
Rais Mteule Mutharika alisisitiza kuwa, katika kipindi cha utawala wake
atahakikisha kuwa anaifanyia makubwa Malawi sambamba na uhakikisha kuwa
anaifanya Malawi itimize majukumu yake ya kimataifa kufuatia kutambua kuwa
kujitenga kunaweza kuifanya Malawi kutonufaika na fursa zilizopo duniani.
“Nchi
hii ipo katika dunia na siyo rahisi tena kuwa na fikra kwamba Malawi inaweza
kubaki peke yake kama kisiwa. Tunahitaji kuwa na wenzetu wa kusaidia maendeleo
ya Malawi. Tunawahitaji wahisani toka Kusini ama Mashariki, tunayahitaji
mataifa tajiri na mataifa yanayoendelea. Tutafanikiwa sana kama tutaendeleza
urafiki kwa wote. Tufanye hivi bila kujali kuwa sisi ni taifa kwani hali ya
sasa inahitaji kila mmoja wetu kushirikiana na mwenzake,” alisema.
Katika
hotuba hiyo pia amesisitiza kuwa kipindi chake cha utawala atajitahidi
kukabiliana na rushwa na kwamba hatakuwa na mchezo kwa wala rushwa katika
kipindi akiwa madarakani. Pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa kuiunganisha Malawi
kwa miundombinu bora ili kuboresha maisha ya wananchi sambamba na kusogeza
huduma za wananchi karibu.
Rais
Mutharika aliapishwa juzi baada ya kuwashinda washindani wake akiwemo Rais
aliyemaliza kipindi chake Joyce Banda ambaye hata hivyo hakuweza kutokea katika
sherehe hizi za kukabidhi madaraka. Akizungumzia suala la kutohudhuria kwa Rais
Banda, Rais Mteule Mutharika alisema alitegemea Rais Banda kuwepo lakini
hakufika nay eye anatambua kuwa wakati wa uchaguzi kulikuwa na tofauti baina
yao lakini kwa sasa uchaguzi umeisha na amesahau yaliyopita ili kuanza ukurasa
mpya wa kuijenga Malawi. Katika shughuli hiyo pia Rais wa zamani wa Malawi
Kamuzu Banda alihudhuria.
Makamu
wa Rais Dkt. Bilal na msafara wake walitarajiwa kurejea nyumbani leo hii
Jumatatu mara tu baada ya kukamilika kwa kazi hii ya makabidhiano.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Juni 02, 2014 Blantyre, Malawi
No comments:
Post a Comment