Monday, June 9, 2014

POSHO NI TATIZO KILA PAHALA EH?



Wachezaji wa Cameroon wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kucheza na Ujerumani


KIKOSI cha Cameroon leo kimegoma kupanda ndege kwenda Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia ili kushinikiza malipo ya posho za kushiriki michuano hiyo.

Timu hiyo imebaki katika hoteli yao mjini Yaounde, wakati Waandishi wa Habari walikuwa nje ya ofisi za Shirikisho la Soka Cameroon kupata maelezo juu ya sakata hilo.

Ndege ilitarajiwa kuondoka Yaounde Saa 3:00 asubuhi kwenda Brazil, wakati Cameroon inacheza mechi yake ya ufunguzi Ijumaa na Mexico.
 
Wachezaji wa Cameroon wiki iliyopita walitaka kugoma hadi kwanza
wapewe posh zao, lakini wakasitisha mgomo huo na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani Jumapili iliyopita, liliripotia gazeti la L'Equipe la Ufaransa.
 
Cameroon ipo Kundi A na wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.


No comments:

Post a Comment