Tuesday, June 3, 2014

NITAPELEKA USHAHIDI ROMA KUHUSU MAISHA YA NYERERE - MUSEVENI




Rais Yoweri Museveni akihutubia waumini waliohudhuria ibada hiyo.
 

Baadhi ya Watanzania wakiwa katika ibada ya kuombea mchato huo.

Watanzania wakifurahia jambo
 Ibada ikiendelea

Mwili wa Kristo? amina.
 Waumini wakifuatilia kilichokua kikiendelea
Mama Maria Nyerere alikuwepo
Salamu mama.


Na Paul Mallimbo, Kampala, Uganda:

 Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni  amesemakiongozi bora ni Yule anayefuata maagizo ya Mungu na kuwatumikia binadamu wote kwa usawa  na haki.

Rais Museveni aliyasema hayo (Junimosi)    wakati wa ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya hayati   Baba waTaifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenye heri na hatimaye kutangazwa mtakatifu.
Alisema hata kwenye maandiko matakatifu ya Biblia kuna mistari inayomtaka binadamu ampende binadamu mwenzake kama anavyojipenda yeye.

“Kwenye biblia kuna sehemu inauliza kuwa utampendaje Mungu ambaye hujawahi kumuona, na ushindwe kumpenda binadamu mwenzako,”

Alisema kwasababu aliwahi kufanya kazi na mwalimu, anaweza kutoa ushahidi kwamba mwalimu alifanya yote mawili, kumtii Mungu na kuwatumikia binadamu.

Alisema moja wapo ya sababu iliyomfanyaHayati  Papa Paulo II kutangazwa mtakatifu kuisaidia UlayaMashariki, ambayo wananchi wake walikuwa hawamwamini Mungu.

“Marehemu Papa Paulo IIalisaidia kuikomboa Ulaya Mashariki kutoka kwenye ukomunisti,wananchi walikuwa hawaamini kuna mungu, lakini kwajuhudi zake aliwafanya wamwamini na kumpenda Mungu,”alisema.

Rais Museveni alisema anatarajia kupeleka ushahidi kwaPapa Francis kwamba Mwalimu ana sifa za kutangazwa kuwa mtakatifu kwasababu alimtii Mungu na kuwatumikia binadamu.

“Miminitapelekaushahidikwa Papa,   kwamba mbali na mwalimu kumtii Mungu na kuwapenda binadamu wote, pia aliwakomboa Waafrika kutoka Ruvuma  mpaka Capetown, huu ni ukweli siyohadithi, alisisitiza Rais Museveni.

Kufuatia hatua hiyo ya kwenda  Roma kutoa ushahidi, Rais Museveni amesema katika maadhimisho ya kuombea mchakato wa Mwalimu kuwa 
Mtakatifu yatakayofanyika mwakani, ameahidi kuwaita maraisi wote waliowahi kufanya kazi na Mwalimu  Nyerere ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa Hayati  Baba waTaifa ameweza kuwaunganisha Waafrika.

Alifafanua kuwa Mwalimu ametoa mchango mkubwa wa ukombozi kwa nchi za Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Namibia, Angola, AfrikaKusini, Uganda  na     Tanzania yenyewe.Hivyo kuja kwa viongozi hao kushiriki ibada hii itakuwa  Baraka kubwa.

Rais Museveni ambaye alitumia muda mwingi wa hotuba yake kuzungumza  Kiswahili, alisema baada ya jitihada za mwalimu kuikomboa Uganda, ndipo na wao walipoweza kuzisaidia nchiza 

Rwanda, Sudan Kusini na Congo kujikomboa na kuongeza kuwa kama sijuhudi za mwalimu wasingekuwa na uwezo wakuwasaidia wengine.

Aidha Rais huyo wa  Uganda ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, alisemakuwa, kwa upande wa viongozi weusi, hakuna kiongozi ambaye ametoa mchango mkubwa kama Marehemu Mwalimu Nyerere.

“Hapa Duniani sidhani kama kuna mtu mweusi mwingine ambaye ametoa mchango kama mwalimu, na hili nimelishudia mwenyewe sikuambiwa na mtu, aliongeza kuwa, hata mzee wetu Nelson Mandela alifanya kazi kubwa Afrika ya Kusini lakini Mwalimua lifanya kazi kubwa zaidi ya ukombozi waAfrika, Alisema.

Alisema Mwalimu aliikomboa Tanzania na kuwafundisha diniya Kristu, kwa vitendo siyo kwa maneno. Aliongeza kuwa nchi nyingine za Afrika zimepatwa na machafuko ya ukabila na dini kutokana na msingi mbaya wa viongozi waliotangulia.

“Tanzania  ninchi ya Wakristo, Waislamuna wale wengine wanaoamini dini za kienyeji lakini mwalimu aliwafundisha Watanzania fikra za kizalendo za umoja,alisema .

Alisema  Uganda  haikupata elimu nzuri juu ya jambo hilo, viongozi wa kwanza wa taifa hilo waliwapandikiza wananchi chuki, kwamba dini ni kumchukia mwenzako, waumini wa dini moja kuwa chukiawaumini ya dini nyingine na matokeo yake niumwagaji wadamu.

“Biblia inasema kile unachopanda ndicho unachovuna, kwahiyo sisi hapa tulipanda mbegu mbaya na tukavuna umwagaji wadamu,” alisema nakuongeza kuwa Tanzania haijawahi kuona umwagaji mkubwa wa damu zaidi ya ajali za magari na ile ya kipindi kile wakati askari wa 

Tanzania walipokwenda  Uganda  kupigana na Idd Amin, Nadhani hii ndiyo damu pekee mmeona,” alisema.

Alisema baadhi ya waasisiwa  Uganda waliwafundisha kuwa wakristu kuwachukia Waislamu, matokeo yake nchi imekuwa katika umwagaji wa damu tangu ilipopata uhuru. Aliongeza kuwa mpaka 1986 wakati anaingia madarakani raia 800,000 wa Uganda walikuwa wamekufa kutoka na chuki za udini na ukabila.

“Uganda imeshuhudia umwagaji mkubwa sanawadamu, Congo wameona damu, Sudan, Somalia,Kenya, Rwandana Burundini Tanzania pekee ambayo imekuwa kama kisiwa cha amani, hii yote nikutokana na mchango wa mwalimu Nyerere ambaye alidumisha amani, umoja na maendeleo kwa watu wake.

Alisisitiza kuwa, sababu moja ya kumfanya mtu awe mtakatifu ni watu kutoa ushahidi wa matukio mbalimbali yaliyofanywa na mtu huyo wakati wa uhai wake, aliahidikwenda  Roma  kutoa ushahidi kuhusu matendo ya Baba waTaifa Mwalimu Nyerere.

“Nikienda kwa Baba Mtakatifu, Papa Francis nitatoa ushahidi mzuri juu ya marehemu Mwalimu Nyerere tena nitatoa kwa maandishi siyo kwamaneno pekee yake”alisisitiza.

Ibada ya kumuombea  Baba waTaifa ilifanyika katika Kanisa la Mashahidiwa  Uganda, Namugongo ambapo ibada hiyo iliendeshwana Askofu Mkuu wa Jimbo  la Kampala, Dk. Cyprian  Kizito Lwanga, ambaye aliiomba serikali kusaidia kuboresha eneo la kanisa hilo ili liwe na miundombinu ya kisasa zaidi.

Hii ni mara ya nane ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya  baba wa Taifa kuwa Mwenye heri na hatimye mtakatifu unafanyika katika kanisa hilo nchini  Uganda. Mchakato huo ulianza mwaka 2006.

Katika ibada hiyo ambayo imehudhuriwa na maelfu ya Watanzania,pamoja na mataifa mbalimbali duniani, pia ilihudhuriwa na familia ya Marehemu Baba waTaifa, Waziri Mkuuwa Uganda Amama Mbabazi mawaziri na wabunge kutoka  Uganda,ambapo Tanzania iliwakilishwana Balozi wa  Tanzania  nchini Uganda.



No comments:

Post a Comment