Wednesday, February 26, 2014

DIDIER DROGBA USO KWA USO NA KOCHA WAKE WA ZAMANI




Didier Drogba (kulia) akiwa na kocha wake wa zamani José Mourinho 
(kushoto)
 

Mshambuliaji wa klabu ya Galatasaray kutoka Cote d'Ivoire, Didier Drogba ameelezea furaha yake kuona anakutana uso kwa uso na meneja wake wa zamani José Mourinho, akibaini kwamba klabu ya Chelsea ilikua bora mara kumi kuliko klabu anayoichezea ya Galatasaray, kabla ya mzunguko wa 8 wa mchuano wa kwanza katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Mshambuliaji huyo, mwenye umri wa miaka 35, ambaye aliichezea Chelsea kwa kipindi cha miaka minane, kati ya mwaka wa 2004 hadi 2012, amebaini kwamba chelsea ilikua klabu bora, hata wakati alipokua akiichezea.

“Nadhani kwamba Chelsea inaweza kufanya vizuri, hata kama ni vigumu kushinda. Kama nacheza, ni kutaka kushinda. Lakini itakua vigumu kwa chelsea. “Hata Juve pia ilikua bora kuliko sisi, kwa hio hali kama hio hutokea”, amesema Drogba.

“Itanitia uchungu na ntashindwa kucheza vilivyo tutakapo kutana na Chelsea, amesema Drogba” ameendelea kusema Drogba, akibaini kwamba anafurahi kwa haki aliyoitendea klabu yake ya zamani.Didier Drogba, amempongeza kocha wake wa zamani, José Mourinho, akibaini kwamba uhusiano wao ulikua mzuri, na ataendelea kumheshimu.

Meneja huyo wa Chelsea, José Mourinho, alimuomba mara kadhaa Didier Drogba, kujiunga na klabu yake ya zamani ya Chelsea, lakini mshambuliaje alikataa na kumthibitishia meneja wake wa zamani kwamba hawezi kuachana na klabu ya Galatasaray, jambo ambalo liliwafanya viongozi wa klabu hio kuwa na imani na Drogba.


No comments:

Post a Comment