Facebook na WhatsApp ni
maarufu sana miongoni mwa vijana.
Kampuni ya mtandao wa
Kijamii ya Facebook imesema kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe
mfupi wa WhatsApp kwa kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya
dola bilioni tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na
wafanyikazi wake.
Hiyo ndiyo biashara
kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa.WhatsApp
ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya
kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.WhatsAp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji
milioni mia nne hamsini.
Katika taarifa,
mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani
kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa.
No comments:
Post a Comment