Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) Assah Mwambene, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy (mwenyeshati la mistari) na
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Prof. Hermas Mwansoko (katikati) wakimkabidhi kiroba cha mchele moja ya
Wazee wa Kituo cha Mwanzange Mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa
na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali katika kikao kazi kinachoendelea
Mkoani humo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko akimkabidhi Afisa Ustawi wa
Jamii anayesimamia kituo hicho cha wazee Bi Otilia Daniel fedha za kununulia
mahitaji mengine wakati wa ziara ya kutoa msaada katika kituo hicho leo Mkoani
Tanga.
Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wazee wa kito cha Mwanzange ambapo walitoa Unga
sembe Kilo 200,mchele kilo 300,mafuta ya kupikia dumu 2,mafuta ya kupaka, dawa
za meno, chumvi, sukari, maharage, nyama, majani ya chai, kanzu, misuli pamoja
na nguo za kinamama. (Picha Na Hassan Silayo)
No comments:
Post a Comment