Picha juu na chini ni
Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet
akizungumza na wanafunzi wa shule za sekondari mbalimbali za jijini Dar es
Salaam na kuwaonyesha picha na kuwapa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ambayo
wakinamama wamekuwa wakifanya kwa mustakabali kwa kuleta usawa na haki za
wanawake duniani.
Shirika la Ufaransa la
Alliance Francaise de Dar es Salaam liliandaa safari ya maonyesho iliyopewa
jina “women in Resistance by the talented French photo-journalist Pierre-Yves
Ginet.
Mwandishi wa habari
huyo mpiga picha Pierre-Yves Ginet ambaye alifanya kazi ya kutafuta wanawake
wanaojituma katika maisha yao ya kila siku na kazi zake zimeweza kuwapa ari na
moyo wakinamama wengi Afrika.
Kati ya 2001 na 2006,
alisafiri zaidi ya nchi 17 akipiga picha za wakinamama ambayo katika shughuli
zao waliweza kufungua ukurasa mpya na kubadilisha historia katika kizazi cha
leo.
Katika shughuli na
katika njia tofauti walizotumia katika kubadilisha maisha wa wakinamama wengi
duniani, wanawake kupitia kazi za picha Ginet wameweza kuwa na dhamira moja
kubwa nayo ni kubadilisha maisha ili kuweza kuwa matumaini ya kuwa na maisha
bora zaidi kwa sasa na baadaye.
Maonyesho hayo ya lengo
la kuwapa usawa wakinamama wote kupitia mabara yote hapa duniani na hasa nchi
zinazoendelea, sehemu za vita.
Na sehemu kubwa ya
picha hizo zinaonyesha jinsi wakinamama wanavyopambana ili kujikwamua katika
unyonge na
ukandamizaji wa aina
yoyote hapa duniani.
Mmoja wa wananfunzi akibadilishana mawazo na Mwandishi wa habari na
mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet anayetumia maonyesho ya picha
mbalimbali kuelimisha jamii kupitia picha .
Afisa Habari kutoka
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama
akifafanua jambo kwa wanafunzi wa shule za sekondari mbalimbali za jijini Dar
es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji
duniani.
Ujumbe wa Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji
duniani inayoambatana na siku ya Wanawake Duniani ni kufikisha sifuri katika
kuondoa swala ukeketaji duniani.
Ujumbe unasema kwamba
ukeketaji umepungua katika sehemu kubwa ya dunia na takwimu zinasema kwamba
zaidi ya wanawake na wasichana 125 milioni ambao wanaishi katika dunia ya leo
katika nchi 29 za Afrika na Mashariki ya kati walifanyiwa vitendo vya
ukeketaji, na kama swala hii likiendelea zaidi ya wasichana 86 milioni duniani
watafanyiwa vitendo vya ukeketaji kufikia mwaka 2030
Hizi ni baadhi ya picha
za wanawake nchini Tanzania ambao wameleta mabadiliko katika maisha yao na
wengine hapa nchini.
Baadhi ya picha
zinazoonyesha matukio mbalimbali yaliyokusanywa na Mwandishi wa habari na mpiga
picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet.
No comments:
Post a Comment