Kiukweli kabisa! si kila mtu anayeiweza hii sanaa ya jicho! kuchonga nyusi iendane na jicho la mhusika! si wote! wengi huwa wanaharibu muonekano wa jicho la mtu!
kutoka ndani ya nafsi yangu ningetamani mi kuwa na uwezo wa kumchonga mtu nyusi akapendeza kama huyu ,ingawa huwa nawachonga baadhi ya watu ambao huwa wanaamini nawapatia! lol
kope sasa! hilo jicho hapo juu limekubalije? hapo limefumbwa! likiinuliwa weee! utadhani anakwita kumbe anakutazama tu. eye shadow imekubali na kope zimebandikwa vizuri mnppp! hapo ndo nnapotamani kubandika ila nikifikiria gundi! mh naishiwa nguvu! big up kwa wale wanawapatia watu kuwapaka eye shadow ,kubandika kopa na kuchonga nyusi! ambao bado si vibaya kujifunza na kufanya vizuri zaidi!
jumatatu njema.
No comments:
Post a Comment