Tuesday, April 24, 2012

Mambo ya SIMU

Mambo vipi wadau? mu wazima? 

Nilikua katika ibada ya misa jumapili fulani kanisani kwetu parokia ya mt Peter Clavery, na Padri Marlan Rodrigez alihubiri juu ya  matumizi ya simu na wapenzi ama wana ndoa wanapowashirikisha watoto na kukurupuka pindi warudishiwapo ujumbe! najua unaweza kua hujanielewa, ilikua hivi! kulikua na familia moja baba yuko kazini na mama yuko nyumbani na mwanawe mdogo alimuomba mama yake amnunulie vitu kaka matunda,pipi na chips kuku  basi mama akamwambia mwanawe mdogo! mpigie baba yako umuombe vitu hivyo! mtoto akaomba awekewe namba kwenye uso wa simu ya mama yake. baada ya simu kupigwa! ikasikika sauti ya mwanamke upande wa pili ikijibu simu unayo piga haipatikani kwa sasa, mtoto mbio mama baba hapokei lakini kuna mwanamke aliyepokea! mama ake akapagawa akaanza oh subiri atanikoma leo akirudi

baba kurudi akakuta mkewe ametutumka kama ametiwa hamira! ile anatoa salamu tu! ana kibao,ngumi, baba akabutwaika haya kuna nini yote haya tena mbele ya mtoto? ma a ehee leo ulimpa mwanamke wako simu aongee na mimi ili iweje? mume mh mimi? mwanamke? hapana, mtoto alipoulizwa akamjibu ndio nimemsiki mwanamke, mume akafikiri weee akagundua kuna wakati alitingwa na kazi hivyo hakupokea simu ya mkewe lakini baadae aliiona miss call ya mkewe! basi alimuelekeza na kweli akasikia simu ikiita bila majibu na sauti ya kike ikajibu! SIMU UNAYOPIGA KWA SASA HAIPATIKANI!  akaelewa na kuomba radhi.
lakini ni wangapi kati yetu katika mahusiano huwa tunayababe na kuyachukulia kweli na kuanza kugombana na wapendwa wetu! tafakari kabla ya kuchukua hatua. siku njema

No comments:

Post a Comment