Tuesday, April 24, 2012

Wivu wa Mapenzi Amuunguza Kwa Pasi ya Moto Mkewe

NewsImages/6373006.jpg
Mke wa Henry baada ya kuunguzwa vibaya na moto wa pasi
Mwanaume mmoja wa nchini Nigeria anashikiliwa na polisi kwa kumuunguza na pasi ya moto mkewe sehemu mbali mbali za mwili wake zikiwemo sehemu zake za siri kwa kile kilichodaiwa mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na baba yake mzazi.
 
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Henry Nnamdi mkazi wa jiji la Lagos nchini Nigeria, alimuua mtoto wake mchanga kwa kukibamiza kichwa chake kwenye sakafu mpaka alipofariki.

Henry hakuishia hapo alimchukua mke wake wa ndoa yao ya miaka miwili na kumfunga na kamba kwenye kiti kabla ya kutumia pasi ya moto kumuunguza mkewe sehemu mbali mbali za mwili wake.

Henry alimuunguza vibaya mkewe kwenye matiti yake na sehemu zake za siri na sehemu mbali mbali za mwili wake kiasi cha kumfanya mkewe apoteze fahamu na hajazinduka hadi sasa.

Chanzo cha yote ni wivu wa Henry kuwa mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na baba yake Henry na kwamba huyo mtoto wake mchanga si mtoto wa damu yake kibailojia.
Henry anamtuhumu baba yake mzazi kutembea na mkewe.

Tukio hilo lililoutikisa mji wa Lagos, lilitokea wakati wa sherehe za pasaka mwezi huu ambapo majirani wa kitongoji cha Okota walishtushwa usiku usingizini na kelele za kuomba msaaada za mke wa Henry aliyejulikana kwa jina moja la Nnamdi.

Mke wa Henry huku akilia kwa uchungu wa maumivu ya kuunguzwa na moto wa pasi, aliwaita majirani waje kumuokoa.

Baada ya majirani kusita sita kuingia ndani ya nyumba ya Henry, walilazimika kuvunja mlango na kuingia ndani baada ya kelele za maumivu za mke wa Henry kuzidi.

Waliyoyashuhudia ndani baadhi walishindwa kuyangaalia kwa mara ya pili waligeuza njia na kurudi walikotoka na kwenda kuwaita polisi.

Polisi waliwahi kufika na kumkuta mke wa Henry akiwa amezimia hajitambui na maiti ya mtoto wake mchanga ikiwa kwenye sakafu.

Henry alikamatwa na kutiwa mbaroni huku mkewe akiwahishwa hospitali ambako madaktari hadi sasa wanapigania maisha yake ingawa bado fahamu zake hazijamrudia.

No comments:

Post a Comment