habari za jumatatu ya leo! kila uchao jinsi ya kike inajaribu kupata vitu vya kuukana uzee na kuuamsha uso ili tu kuonekana na jinsi me! ingawa urembo wa sasa si wazamani wa mama zetu kuweka majaribosi masikioni kisha baasi imekwisha! lah hasha siku zetu tunaikosoa kazi ya Mwenyezi kwa kuongeza vitu!
nianze na jicho! wanasema mwana mke reception babu! lakini kiukweli jinsi reception hiyo inavyo andaliwa ili kua na mvuto! wakati mwingine huleta madhara! mfano ni hizi kope za kuongeza!
1- aliyeweka kope sharti la kwanza asiziondoe mwenyewe!
2- nina wasiwasi na gundi itumikayo kwani rafiki yangu aliweka kiasi cha kunitamanisha nami nitake kuweka nikasita kutokana na rafiki yangu kuwashwa sana macho ,yakaanza kujaa maji, kuvimba na hatimaye kutoka usaa kopeni! alikuja kuponea hospitali!
sasa enyi muwekao kope ni kwa faida ya nani na huku maumivu kwa baadhi yenu ni dhahiri!? mwisho aloweka kope kulia kwake awapo msibani ni kwa mashaka akilinda kope zake zisinyofoke! lol niwieni radhi urembo wenye madhara na masharti mi siuwezi waungwana. kesho naja na midomo. jumatatu njema yenyee kijimvua mvua.
siku njema...
No comments:
Post a Comment