Leo ni siku ya mapumziko kwa walio wengi na wachache huenda kazini kama kawaida japo iwe nusu siku! nataka niwaangalie wanawake wafanya kazi walioko katika miji mikubwa! wao kwao leo ni siku ya usafi wa miili yao.kucha na miguu kusuguliwa! hilo halina tatizo! mi nachoshwa na huu urembo wa nyongeza. kope, tatoo, na midomo!
huwa tuna sema kazi ya mola haina makosa! sasa iweje watu waikosoe kazi ya Mungu? kwa kuongeza vitu? hii ina maana gani? na kwa faida ya nani? kama wewe mzuri mzuri tu! mnisamehe maana namimi pengine mshamba! ila madhara yapo! mkubali ama mkatae habari ndo hiyo! tuanze na kope
kope za wenyewe lol
siwasemi mnaoziweka hapana! najaribu kuwaza kwa sauti tu! kwa raha zenu? ama kwa faida ya nani? ninao marafiki wanao ziweka hizo ila sina jibu la moja kwa moja. nlipotaka kubandika, nikaogopa kutokana na rafiki zangu wawili waliwahi kuweka wakaumia! sasa sijui muwekaji fake? au gundi ndo feki? nikaona isiwe taabu.
nyusi za tatoo
sijui ni kutokua na muda?au ninini wanawake wameamua kunyoa nyusi zote na kubaki kipara na kisha mashine ama sindano kupita juu ya nyusi zao na kuchora mchoro usio toka milele! next time ntakuletea tatoo za wanaume na mvuto wake.
kama hiyo haitoshi wanawake naona wamechoka kupaka paka lipstick zinazotoka basi wameamua kuchora midomo tatoo za rangi mdomoni kuepusha usumbufu ,ila najiuliza je ukienda msibana na tatoo ya rangi ya mdomo na nyusi zimechorwaa? waswahili watakufikiriaje? najua watoto wa mjini hawajali na misiba sasa hivi sio kiviile kama zamani.
huu mdomo ndo ushachorwa kazi kubwa ni lipbam au lipshine!
umeona bana! inapendeza kiukweli
wino unaohusika midomoni na mwilini hiyo ni red kala! lol
well pendezeni wanawake wenzangu, hiyo huongeza confidance kiukweli! jumamosi njema.
No comments:
Post a Comment