Kampeni ya Stand up fo African Mothers itadumu kwa miaka 3, lengo ni kutambua na kuthamini mchango wa wakunga ,na hasa katika kuwawezesha ki elimu na hata kupata tuzo, mmoja wapo ni mkunga kutoka Uganda Ester Madudu anayewania tuzo ya Nobel.
je unaweza ku Stand Up For African Mothers? ni rahisi basi unaweza kusaini petition kupitia link hii http://www.standupforafricanmothers.com/ utakua umeunga mkono na kuonesha support yako kwa wakunga na kuwapa sauti serikali na mashirika ya kimataifa katika kampeni hii.
lengo la ukusanyaji huo wa saini ni kufikisha saini 1,000,000 kutoka kwa watu wote ulimwenguni ambao watasimamia wanawake wa Africa. wale wote wenye mapenzi mema wanaalikwa kuwasaidia wakunga wa Tanzania mafunzo ili wapate elimu ya awali ya afya,vitendea kazi vinavyohitajika ili kuweza kupunguza vifo vya uzazi Africa,ki ukweli mtoto hapaswi kuachwa yatima na mama yake hapaswi kufa wakati yeye analeta uhai kwa kutokana na huduma duni za afya ama mkunga kutokua na uwelewa wa kazi afanyayo.
mkunga mmija akielimishwa anao uwezo wa kutoa huduma kwa wazazi wapatao 500 kwa mwaka.
AMREF ni asasi ya kwanza ya Afya Africa kuwa na kampeni ama mpango mkakati wa namna hiyo na lengo lao kuu ni kuwasomesha wakunga 15,000 mpaka kufikia mwaka 2015 ili kupunguza vifo vya uzazi kwa asilimia 25.
Endapo hatutatilia mkazo na kutoa elimu kwa wakunga na kutotoa unuhimu unaostahili kwao hasa katika nchi zinazo endelea mwamko wa wakunga utakufa na hivyo kusababisha mzigo mkubwa kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara ambako:-
-kila mwaka wanawake 200,000 hufa kwa kukosa huduma rahisi.
-watoto wa ki Africa wapatao milioni 1.5 huachwa yatima kila mwaka.
-wanawake asilimia 70 hawapati huduma stahili za uzazi na nusu ya wale wanaojifungua,hujifungulia majumbani bila uangalizi na mbaya zaidi asilimia 95 ni kutoka Southern Sudan
JE HUONI SABABU YA KU STAND UP FOR AFRICAN MOTHERS? WEKA SAINI YAKO UWE MMOJA WA WALE WANAOJALI AFYA YA MAMA NA MTOTO NA KUPINGA VIFO VYA AKINAMAMA WANAOJIFUNGUA NA KUACHA WATOTO YATIMA.
KWA MAELEZO ZAIDI INGIA www.amref.org
mgeni rasmi ni Mama Salma Kikwete.
No comments:
Post a Comment