Jana nilipata meseji ifuatayo kutoka kwa Wastara...Habari ndugu yetu mpendwa tumefika salama tunashukuru Mungu.Nimechelewa kupata line ndio maana nimechelewa kuwasiliana na wewe.
Nikamjibu...Nafurahi kusikia mmefika salama mmeshaenda hospitali direct?hospital inaitwaje?hatua za awali madaktari wanasemaje?
Akanijibu...Inaitwa Saifee iko Mumbai na huku wamemrudia tena vipimo ili kujua waanzie wapi.Ila dada kuna tatizo limetokea huko nyumbani Tanzania kuna matapeli wanaifata familia huko na kujifanya wao ni waganga wanataka kumtibia Sajuki.Wanataka wapewe ml 3.5 wamuopoe Sajuki maana kalogwa na mtu aliyemzulumu.Na kiukweli sisi hatujawahi mzulumu mtu.Wapo wengi hao wanaisumbua familia kweli toka tumeondoka naomba uwakanye kupitia kipindi waache hiyo tabia si nzuri wanatukwaza sana.
Nikamjibu.....sawa dada usijali i will adress hiyo ishu kama wakisikia watajua wameshtukiwa.Haya kila la heri tutazidi kuwasiliana.
Akajibu sawa asante dada!
No comments:
Post a Comment