Donna Summer
Mwanamuziki Donna Summer amefariki dunia , na enzi za uhai wake alipata umaarufu mkubwa kwa vibao vya disco kama I Feel Love, Love To Love You Baby na Love's Unkind, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63.
Familia ya mwanamuziki Donna Summer imetoa taarifa kwa umma juu ya ratiba ya maziko ya malkia wa disko kua itakua jumatano ijayo huko Neshville.
Na yote hiyo inakuja kwasababu familia hiyo ilihamia katika mji huo mwaka 1994,na imeuchagua mji huo kwasababu ndio mji wa nyumbani na ulikua ndani ya moyo wa mwanamuziki huyo muda wote na kihistoria Nashville ni mji wa kitamaduni katika tasnia ya muziki duniani hivyo akizikwa huko italeta maana.
Malkia huyo aliaga dunia huko Florida kutokana na ugonjwa wa kansa ya koo.Bwana ametoa ,Bwana ametwaa jina la Bwana limarikiwe.Amina.
Malkia huyo aliaga dunia huko Florida kutokana na ugonjwa wa kansa ya koo.Bwana ametoa ,Bwana ametwaa jina la Bwana limarikiwe.Amina.
Diva Summer alikuwa ni miongoni mwa wasanii mashuhuri sana wa mtindo wa disco aliyewahi kutunukiwa tuzo tano za Grammy kati ya 1978 na 97.
kwa ushirikiano mkubwa na Producer Giorgio Moroder katika kuimarisha mtindo wa disco duniani kote.
mahali alikozaliwa walimbatiza jina la LaDonna Andre Gaines, alikulia mjini Boston na alianza kuimba katika kwaya ya kanisani kwake katika viunga vya Boston.
Donna Alianza kuimba katika tamthilia ya muziki Hair katika miaka ya mwisho ya 1960 nchini Ujerumani ambako hatimaye ndiko alikoamua kuyamalizia maisha yake.
Rekodi yake ya kwanza aliitoa mwaka 1971 kutokana na ushirikiano wake na msanii wa Kitaliana Moroder ndio uliomletea umaarufu kwa kibao maarufu cha Love to Love You Baby mnamo mwaka 1975.
No comments:
Post a Comment