Monday, May 28, 2012

Mtumishi wa Papa Benedict akamatwa


Basillika hiyo.



kwenye duara ni mtuhumiwa Paolo Gabriele akiwa na Bosi wake Papa Benedict wa xvi



Jana ilikua ni siku ya kumuabudu Mungu kwetu sisi wakristu, wengi walijitokeza katika nyumba za ibada, kwa wakatoliki kama mimi mkuu wetu ni Papa Benedict wa xvi, makao yake makuu yako Roma nchini Italia.kuna jambo huko mjengoni ambapo ,Polisi wa Vatikani wamemshtaki rasmi mtumishi wa Papa Benedict, katika kesi inayohusu wizi wa nyaraka za siri.
Paolo Gabriele - ambaye alikua akitumika kwenye fleti ya papa - amezuwiliwa Vatikani, na ameruhusiwa kuonana na mawakili wawili.
Wakuu wanachunguza vipi, katika miezi ya karibuni, magazeti ya Utaliana yalipata nyaraka ambazo zinaeleza mashindano kati ya wakuu wa kanisa - kisa ambacho kimeanza kuitwa 'Vatileaks'.
Inaarifiwa kuwa Papa Benedict ameshangazwa na kusikitishwa kuwa mtumishi wake mmoja amekamatwa.




Mkuu wa Benki ya Vatikani alitolewa kazini Alhamisi, kutokana na kashfa hiyo.

No comments:

Post a Comment