Thursday, May 3, 2012

Habari Za Dunia yetu-Watoto milioni 15 Huzaliwa Kabla ya Wakati




mtoto njiti

Kila mwaka watoto milioni 15 wanazaliwa kabla ya wakati kote duniani ikiwa ni zaidi ya mtoto mmoja kati ya watoto 10 wanaozaliwa inasema ripoti iliyotolewa Jumatano na shirika la afya WHO iitwayo "Born Too Soon:The Global Action Report on Preterm Birth
Kwa mujibu wa ripoti hiyo zaidi ya watoto milioni moja kati ya hao wanafariki dunia mara tuu baada ya kuzaliwa, na wengine wengi wanaathirika na maradhi ya muda mrefu ya viungo, mishipa au matatizo ya kusoma na mara nyingi huzipa familia zao na jamii gharama kubwa.
Ripoti inakadiria kwamba asilimia 75 ya watoto hao wanaozaliwa kabla ya muda wao ambao hufariki dunia wangeweza kuishi bila huduma za gharama kubwa endapo kungekuwepo na matibabu na njia za kuzuia watoto kuzaliwa mapema ambazo sio za gharama kubwa na zinazopatikana kwa urahisi duniani.
Takwimu hizi zimeandaliwa na wataalamu zaidi ya 100 wanaowakilisha mashirika zaidi ya 40 ya Umoja wa Mataifa , vyuo vikuu na mashirika mengine. Ripoti hiyo pia ina mapendekezo zaidi ya 30 ya kushughulikia suala la kuzuia na kuwatunza watoto wanaozaliwa kabla ya wakati au njiti ambayo yamo pia kwenye kampeni ya moja wa mataifa ijulikanayo kama "kima mama, kila motto inayoongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

No comments:

Post a Comment