Monday, May 21, 2012

Picha inayomkajeli rais Zuma




Rais Jacob Zuma

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC, kimesema kinachukua hatua za kisheria kulazimisha nyumba moja ya sanaa ambayo inaonyesha picha ya rais Jaocob Zuma, sehemu zake za siri zikiwa nje kuondoa mchoro huo.
Msemaji wa chama ametaja picha hiyo kama inayoudhi, ya kuchukiza na yenye matusi.Mchoro huo ni sehemu ya maonyesho ya michoro mjini Johannesburg yenye kauli mbiu ' Sifa kwa mwizi' na ambayo inajumuisha michoro yenye lengo la kukosoa chama tawala ANC.
Mchoraji wa picha hiyo Brett Murray, alisema kuwa picha zake zinajieleza


Picha yenye utata ndo hiyo hapo na sehemu iliyofichwa katika picha za mtandaoni ziko ambazo ni wazi, lakini kutokana na maadili yetu sisi Wa Tanzania nashindwa kuiweka wazi picha hiyo. angalia kati ya kidole kidoko na cha pete utagundua kitu.



mchoraji



 aliyechora picha ambayo imezua tafrani ni huyo hapo juu. ambaye anadai picha zake zinajieleza! hata asipoweka caption! uh lalalla, duniani kuna mambo!


moja ya kazi za Murray




unaikumbuka hii issue?



kazi zake anaziita hivyo!



hii imezibwa kwa heshima ya baba Zuma.



watu wakiishangaa  na kuipiga picha,picha  hiyo

 

No comments:

Post a Comment