Friday, May 4, 2012

Kutoa Ni Moyo

                                      Sajuki alivyo sasa na alivyokua kabla ya maradhi


Ndugu na mpendwa wetu, mwigizaji mahiri Sajuki kama ulivyosikia katika vyombo vya habari, magazeti na redio kua anaumwa wimbo wake wa  MBONI YANGU  ni maalum kwa ndugu yetu msanii Sajuki ambae anahitaji mchango wako wa hali na mali kuokoa maisha yake. Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini India kwa matibabu.Wimbo  uliorekodiwa  unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe ya MBONI YANGU.Na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo aliuimba Wastara.Wimbo huo umerekodiwa kuhamasishana kuchangia na umeanza kusikika leo hapa clouds fm na video ya tukio zima la kurekodi itaonekana clouds tv.Na leo  hii Dina Marios anategemea kukusanya angalau Tsh ml 12,000,000 hapa clouds fm.Nakuomba sana mtanzania mwenzangu tushirikiane katika hili.
msikilize Dina Marios sasa hivi yuko hewani kuchangisha pesa za safari na matibabu katika 88.4 Clouds Fm, asante Mungu kwa kuwagusa watu wako! mdau wa Clouds Kutoka 92.9 Iringa amekuguswa na amejitoa kiukweli  tena sana tu Dola 5000/-  na Mungu arudishe pale palipopungua kaka ! ingawa mdau  amekataa kutajwa jina lake  asante sana!
go Dina Marios , go Clouds Fm and Clouds Tv, go wadau twende pamoja sasa. Mbarikiwe! ukiguswa kuchangia ama unasitasita nina sala yangu kwako!
SALA
Mungu akupe Certificate ya UPENDO,Diploma ya UVUMILIVU,Degree ya UKARIMU,Masters ya UNYENYEKEVU, na Uzee wako upate PHD ya kumcha MUNGU aliyekuumba. amina.
ASANTE SANA! BE BLESSED

No comments:

Post a Comment