Saturday, May 12, 2012

Ugiriki yashindwa kupata serikali


              Kiongozi wa chama cha kisoshalisti nchini Ugiriki Evangelos Venizelos

Ni ndani ya dakika tisa tu zilizopita! zoezi hilo limeshindwa kufanyika.
Kiongozi wa chama cha kisoshalisti nchini Ugiriki , Evangelos Venizelos, amesema ameshindwa kuunda serikali, akiwa ni kiongozi wa tatu wa chama hicho kushindwa kufikia malengo yake kufuatia uchaguzi wa jumapili.Uundwaji wa serikali ya mseto ulikuwa mgumu zaidi baada ya wapigaji kura kuunga mkono kwa kiasi kikubwa vyama vinavyopinga vikali mipango ya kunusuru uchumi iliyobuniwa kwa ajili ya kupunguza madeni ya Ugiriki.
Mazungumzo yanatarajiwa kuhusu uundwaji wa serikali ya dharura.Kama hilo limeshindikana uchaguzi mpya huenda ukafanyika mwezi ujao.
Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Arthens anasema, hatma ya Ugiriki miongoni mwa nchi za ukanda wa Euro kwa mara nyingine iko mashakani.
Ujerumani inasema Ugiriki haiwezi kuendelea kupokea madeni ya kimataifa, kama serikali yake ijayo haitaafiki mipango iliyobuniwa ya kunusuru uchumi wake.



No comments:

Post a Comment