Wednesday, May 16, 2012

Tashtiti katika Mahaba za nini?



mara nyingi mimi hujiuliza sana kwanini katika mapenzi kuna hali ya kususa, kununiana? hayo ni mambo ya kawaida kama uko kwenye ndoa , ama una mpenzi,boyfriend ama bwana au bibi. inatokea hiyo ni kutaka hisia zako zitambuliwe. sio mbaya kama itadumu kwa muda mfupi na kwisha haraka mara baada ya maongezi kti yenu!
huwa sipendi kuona mtu ana nongwa na kushika bango kwa vitu vinavyozungumzika, na mbaya zaidi mtu huyo anapowashirikisha marafiki zake issue ya yeye na mpenzi wake, mbaya na kubwa kuliko ni pale ambapo mpenzi wake wa kiume ama wa kike anapotokeza mbele za watu mlipo niangalie wanawake zaidi, kwasababu nadhani naweza kuileza zaidi jinsi nilimo(elewa hicho kiswahili hapo,lol)
mwanamke anataka kuonesha kwa marafiki zake amemnunia mpenziwe na maneno na kuweka vikwazo visivyo na sababu kiasi cha mpenziwe kujisikia vibaya mbele ya rafiki wa demu wake, na hujihisi anachoreshwa, jambo la kushukuru labda huyo boyfriend awe na kifua ama ana mahaba ya dhati atakuvumilia vinginevyo anaweza kukuzaba vibao mbele ya rafikizo au kuondoka na kukuacha ukiwa umekaa na shosti zako.
kama una mpenda kwanini mambo ya ndani uyamwage nje? hata kama mbwembwe hizo mnafahamiana ninyi wenyewe kwa watu wa kawaida watakuona wewe mwanamke hukufundwa!
kama unampenda utamjali,kama unampenda hutamfanyia tashtiti hadharani! inaumiza! hata kama amekosa yanini kuita mhadhara? watu hawana dogo watataka kujua kulikoni? then wakasimuliane na waneno ni kama moto nyikani, ukipata mrejesho unatafuta pa kuu weka uso wako!

yanini yote hayo?kama hujui huo ni bonge la mwanya la jamaa yako kutafuta kazi za nje na kubaki na kimuhemuhe, wanawake na wanaume tuache tashtiti katika mapenzi!

No comments:

Post a Comment