Wednesday, May 16, 2012

Vyombo vya Habari bado vinakandamizwa nchini Burundi



Wakati dunia imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari hivi karibuni, kwa taifa la maziwa makuu la Burundi, ilikuwa kama jinamizi. Nchini humo maadhimisho yalighubikwa na sauti kali za wanahabari ambao wanalalamikia utawala kutokana na kuzuiliwa gerezani kwa mwandishi wa habari wa Redio ya kibinfasi na ripota wa Redio ya Kimataifa Ya Ufaransa RFI Hassan Ruvakuki kwa tuhuma za kushirikiana na makundi ya wahalifu wa ugaidi.
Tukio hilo limewafanya wanahabari wengi kujiliza endapo uhuru wa vyombo vya habari una thamani yoyote kwa serikali ya taifa hilo. Wanahisi kushikiliwa kwa mwenzao kunatishia uhuru wa wanahabari lna pia kutia dowa baya kwa Burundi baada ya taifa hilo lilotoka vitani kusifika awali kutokana na vyombo vyake vya habari kuchangia kikamilifu katika mpango wa amani na maridhiano.


No comments:

Post a Comment