Tuesday, May 8, 2012

Kwacha Yashushwa Thamani



                                               
                                             Rais mpya wa Malawi Joyce Banda


Raia nchini Malawi, wamekumbwa  na fadhaa na kukikimbilia kununua bidhaa muhimu , kufuatia hofu ya kupanda kwa bei ya chakula baada ya benki kuu kushusha thamani ya sarafu ya nchi hiyo 'kwacha' kwa 50%.
kufikia mwishoni mwa siku ya jana  , maduka mengi yalikuwa hayana bidhaa kama sukari, mafuta ya kupikia na mkate.

                                                  



                                                         kwacha ya sarafu



                                               
                                                             kwacha mia moja

Thamani ya kwacha, ilishushwa kama sehemu ya mpango wa serikali mpya kutaka kupokea msaada kutoka kwa wafadhili.
Serikali iliyotangulia ilikataa pendekezo la serikali kushusha thamani ya sarafu hiyo ili iweze kupokea msaada.
Watu wanasema kuwa, bidhaa zingine kama, mchele, unga wa mahindi na maji matamu ya machungwa hazipatikni tena katika dukamoja mjini Blantyre la Chichiri, ambalo ndio duka rasmi mjini humo.
Wasiwasi huu umetokea licha ya wachumi kusema hawakutarajia kama kushuswa kwa thamani ya kwacha kungezua wasiwasi huu na kusababisha kupanda kwa bei ya vyakula.
Hata hivyo wafanyabiashara walitarajia hatua hiyo kwani walikuwa tayari wanatumia thamani mpya sarafu hiyo.
Benki kuu ilitangaza kuwa dola moja itakuwa na thamani ya kwacha 250 .

No comments:

Post a Comment