Tuesday, May 22, 2012

Video ya wimbo wa mwisho wa Whtney Houston

Whitney na Jordin  Sparks

Whitney Houston alikua akimpenda sana mwanadada Jordin Sparks na kukubali kufanya kazi naye  amabayo ni ya mwisho kabla ya kifo cha Whitney. na ukiwatazama hao wawili unaoana kabisa jinsi Whitney anavyotazama mbali maana yake si wa hapa tena na Jordin akiwa bado yupo yupo kwanza. huu hapa ni wimbo wao kwa pamoja uitwao Celebrate. ndani Whitney anahamasisha kua its time to celebrate come on and celebrate







Diva, Whitney Houston alifariki February  akiwa na miaka 48, amecheza kama mama yake  Jordin's  walipoigiza filamu iliyowahi kutoka mwaka 1976
Na hiyo ilikua kama anarejea katika tasnia ya filamu baada ya kukaa nje ya ulingo juo kwa miaka 15-, Whitney alikwisha igiza filamu kama The Bodyguard na  The Preacher's Wife.Jordin aliposhiriki katika tamasha la Billboard Awards  , aliimba wimbo wa  I Will Always Love You.
Baada ya kusikia wimbo huo ukiimbwa  Bobbi Kristina Brown akahisi uwepo wa mama yake na akaripuka kilio na hasa pale alipokwenda kupokea tuzo ya  Millennium Award  kwa niaba ya mama yake mzazi.



Bobbi Kristina  anadai kwamba anajiona kua amebarikiwa kua sehemu ya sherehe hizo za kutoa tuzo za Billboard Award  na alitumia fursa hiyo kuwashukuru  watu wote kwa kuwa karibu na familia,kuwasaidia katika nyakati zote ngumu alizopitia mama yake
Na alipanda jukwaani akiwa na meneja wa mamake Patricia Houston huku akilia alitoa shukranin zake  
Na sio kwasababu ilikua nzuri lah hasha pale hali ilipokua mbaya assanteni sana kwa kutuonesha upendo mkubwa na ni kwasababu mama alikua anastahili upendo huo na anashukuru na kusema hatatokea mwingine kama yeye milele.
Whitney  alikufa katika ajali ya kuzama katika beseni la kuogea bafuni a.k.a bath tab na hayo ni matokeo ya ugonjwa wa moyo na matumizi ya dawa za kulevya


Whoopi Goldberg na yeye alitoa mtazamo wake juu ya Whitney Houston  kua ana mheshimu sana na kusema kua waburudishaji wote wanahitaji na wanapaswa kupata upendo na wate mlohudhuria hapa mnampenda Whitney na hata kama hukuwahi kumuonesha upendo Whitney ,sasa ni nafasi yako kufanya hivyo kwasababu usiku huu ndicho tufanyacho na tunakwenda kumpa upendo mkubwa kuliko the greatest love of all. .  nampenda sana huyu mama jamani hasa katika uigizaji wa filamu ya Sarafina!
 Na wimbo  Celebrate  utaachiliwa huko Marekani August 17

 

No comments:

Post a Comment