Friday, May 4, 2012

Taarifa- Mwaka Mmoja wa Kifo Cha Osama

                                                
                                                    Al marohoom- Osama Bin Laden

Osama akiwa  kivazi cha Kijeshi


 Nyaraka mbalimbali zilizochukuliwa kutoka katika nyumba aliyokua akiishi Osama bin Laden nchini Pakistan zimetolewa hadharani nchini Marekani,ikiwa ni mwaka mmoja tokea kuuawa kwa kiongozi huyo wa Alqaeda.nyaraka hizo zimechapishwa kwenye mtandao na kitengo cha utafiti katika chuo cha Kijeshi cha West Point, nchini Marekani.
Miongozi mwa nyaraka hizo 17 zilizotolewa wazi kwa umma ni pamoja na barua na mawasiliano mengineyo ya ki elekroniki ambayo kwa ujumla ni kurasa mia moja na sabini na tano,za kuanzia mwishoni mwa mwaka 2006 hadi mwezi April mwaka wa jana, muda mfupi tu kabla Osama Bin Laden kuuawa.
Watafiti wa Jeshi la Marekani,ambao walishuhudia nyaraka hizo kutolewa kwa umma wanaeleza kuwa zinaonesha katika moja ya barua zake Bin Laden anapendekeza kushambuliwa kwa ndege zinazomsafirisha  Rais Obama katika ziara zake nchini Afghanistan, na kwamba makamu wa Rais JOE BIDEN atashtushwa na tukio hilo na kushindwa kuiongoza nchi.
 Osama Bin Laden alikua na uthubutu wa ajabu wa kuweka bayana mipango yake ya mashambulizi na kisha kufanikisha mashambulizi hayo bila kizuizi.

No comments:

Post a Comment