Sasa wanawake wapendao
urembo na kuongeza mvuto wa mapenzi wanakwenda mbali, nasema hivi kwasababu,
wapo walotoboa kila sehemu yam iili yao na kuweka kitu cha kipekee ili kuongeza
mvuto wa kimapenzi badala ya kwenda kwa mganga!
Mapenzi mengine mabaya!
Watu wanakosa nidhamu,binti mmoja mfanyakazi katika club ya usiku katika jiji
la New York aitwaye Lucy Luckayanko,mwenye asili ya Rusiia, ambaye ana umri wa miaka 25, alifanyiwa upasuaji wake wa
kwanza na kuwekewa kipande cha dhahabu chenye umbo la kopa kwenye kona ya jicho
lake na kila anapoangalia ama niseme atazamo juu mwanga wa jua unapopiga jicho
lake kuna mwanga hutokea kama miale na mng’aro wa kuvutia,kutoka kwenye macho
yake yenye kope ndefu za kutosha! basi ikamvuta mwanamume mmoja, na kumtokea binti huyo.
Dr. Emil Chynn ndiye
aliyefanya upasuaji huu na kumuwekea binti huyo kipande hicho cha dhahabu
katika eneo Park Avenue huko Manhattan wiki kadhaa zilizopita kwa gharama ya $3,000 na kamera zilikua zinashuhudia zoezi hilo.na
hawakuwa watu wa kamera tu bali hata wapiti njia walishuhudia kwani dk Chynn aliamua
kuifanya operation hiyo
kwenye chumba chenye vioo vitupu na hivyo wapiti njia
walikua wakijionea na binti huyo hakujali kutazamwa wakati zoezi hilo
likiendelea.
lUCY baada ya upasuaji aki hakikiwa.
Baada ya Lucy kufanikiwa
kuwekewa urembo huo wa dhahabu kwenye jicho lake, watu wengine wane waliamua
kumtafuta daktari huyo ili nao wawekewe urembo huo.
Lucy hapendi kabisa
kuwekewa tattoo kutokana na kwamba ni ya kudumu, lakini anaufagilia urembe wake
wa jichoni kua anaweza kuuondoa wakati wowote autakao na ameuweka kwa watu
maalum wa karibu mno na yeye.
JE ni watu wangapi amabo watajitolea sehemu
muhimu mno katika miili yao kwa ajili ya wapendwa mno nao? Je huu ndo upendo? Je
mwanamume anampenda mwanamke wa vitu asili? Ama vya kuongezwa? Utofauti utatoka
wapi sasa unapomkosoa muumba?!
Sipingi mtu chake
apendacho,japo hakina hila macho, kuridhika kuwa nacho,mapenzi kwa hakika huwa
hayaoni yaingiapo moyoni mwa mtu! Atafanya
chochote kumridhisha mpenziwe lakini na penginepo labda mwisho wa mapenzi hayo,
yupo atakaye jutia kwa kujitoa zaidi kwa mwenziwe! Na kwa vyovyote ni MWANAMKE
NDO MHANGA KATIKA HILI!
No comments:
Post a Comment