KAMA ILIVYO ADA LIGI HII ILIENDELEA MWISHONI MWA WIKI HII AMBAPO
LIGI KUU YA ENGLAND NDIO BURUDANI PEKEE YA SOKA AMBAYO MASHABIKI MANCHESTER
CITY SIKU YA JUMAMOSI WALIKUWA NA KIBARUA CHEPESI LAKINI KIZITO WAKATI
WALIPOVAANA NA CRYSTAL PALACE .
KINYUME NA MATARAJIO YA WENGI MANCHESTER CITY WALISHINDA LAKINI
HAUKUWA USHINDI WA MABAO MENGI KAMA ILIVYOZOELEKA WAKIWA UWANJA WA NYUMBANI NA
SAFARI HII LILIKUWA NI BAO MOJA AMBALO LILIFUNGWA NA EDIN JEKO.
MAHASIMU WA MANCHESTER CITY AMBAO NI MAN UNITED WALIKUWA UGENINI
HUKO CARROW ROAD KUCHEZA NA NORIWCH CITY NA KAMA ILIVYOKUWA KWA WENZAO ULIKUWA
NI USHINDI KIDUCHU WA BAO MOJA BILA .
BAO PEKEE LILIWEKWA WAVUNI NA MSHAMBULIAJI DANNY WELBECK
AKIFUNGA BAO LAKE LA NNE KWENYE MECHI NNE.
VINARA WA LIGI HII ARSENAL THE GUNNERS WALIENDELEZA UBISHI WAO
KWA KUWAFUNGA NEWCASTLE UNITED BAO MOJA BILA .
BAO PEKEE LILWEKWA WAVUNI NA MSHAMBULIAJI OLIVIER GIROUD.
KATIKA MCHEZO ULIOFUNGA RATIBA YA MECHI ZA LIGI KUU KWA MWAKA
2013 CHELSEA WALIONYESHA UKOMAVU WAO KWA KUWAFUNGA LIVERPOOL MABAO MAWILI KWA
MOJA .
LIVERPOOL NDIO WALIOANZA KUFUNGA KWA MARTIN SKATOL LAKINI
CHELSEA WALIRUDI MCHEZONI KWA MABAO YALIYOFUNGWA NA EDIN HAZARD NA SAMUEL ETOO.
MOJA YA VITU AMBAVYO VIMETENGENEZA VICHWA VYA HABARI ZA MICHEZO
NCHINI MAREKANI NI MAJERAHA AMBAYO YAMEKUWA YAKIWAKUMBA NYOTA WA TIMU ZA NBA
MARA KWA MARA .
MSIMU ULIOPITA WACHEZAJI DERRICK ROSE WA CHICAGO BULLS , RASO
WEST-BRUK WA OKLAHOMA CITY THANDA NA KOBI BRYANT WA LOS ANGELES LAKERS KWA
NYAKATI TOFAUTI WALIPATA MAJERAHA AMBAYO YALIWAFANYA WAKAE NJE YA UWANJA KWA
MUDA MREFU.
KWA BAHATI MBAYA MAJERAHA KWA WACHEZAJI HAWA YAMEJIRUDIA TENA
MSIMU HUU NA KUWAFANYA WACHEZAJI HAWA KURUDI TENA KWENYE VYUMBA VYA MADAKTARI
NA KUKOSA MICHEZO MUHIMU.
ILIANZA KWA ROSE AMBAYE BAADA YA KUCHEZA TAKRIBANI MECHI KUMI
ALIUMIA GOTI LAKE NA ATALAZIMIKA KUKAA NJE YA UWANJA KWA MUDA USIOJULIKANA NA
HUENDA AKAKOSA MSIMU MZIMA IKIWA MARA YAKE YA PILI BAADA YA KUUKOSA MSIMU
ULIOPITA.
KOBE BRYANT AMBAYE ALIREJEA UWANJANI SIKU CHACHE ZILIZOPITA
BAADA YA KUKAA NJE KWA MIEZI TISA ALIUMIA TENA GOTI LAKE IKIWA NI WIKI TATU
ALIPORUDI UWANJANI NA ATAKAA NJE YA UWANJA KWA MUDA USIOPUNGUA WIKI SITA.
RASO WEST-BRUK NAYE ALIFUATA MLOLONGO UO BAADA YA KUUMIA GOTI
LAKE NA KULAZIMIKA KUFANYIWA UPASUAJI IKIWA NI MARA YA TATU KWA GOTI HILO
KUFANYIWA UPASUAJI .
RASO ATAKAA NJE YA UWANJA KWA MUDA WA MIEZI MIWILI NA ATARUDI
UWANJANI WAKATI WA MICHEZO YA ALL STAR MWEZI FEBRUARI.
KOCHA WA TIMU YA BROOKLYN NETS JEISON KIDD AMELAZIMIKA
KUKANUSHA TETESI ZILIZOGAA KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUWA HAYUKO KWENYE UHUSIANO
MZURI NA WACHEZAJI WAKE .
KIDD AMETOA UFAFANUZI HUO BAADA YA VYOMBO VYA HABARI KUSEMA KUWA
AMEKUWA AKIBISHANA SANA NA WACHEZAJI WAKE HASA BAADA YA KUWALAUMU KWA KUKUBALI
KIRAHISI KUFUNGWA.
BROOKLYN NETS WAMEKUWA KWENYE WAKATI MGUMU WAKIWA WANAPATA
MATOKEO MABAYA TANGU KUANZA KWA MSIMU NA HADI SASA WANASHIKA NAFASI YA MWISHO
KWENYE MSIMAMO WA LIGI.
No comments:
Post a Comment