Pope Francis akivuliwa kofia.naye anatabasamu tu.
Mara nyingi watoto
ambao wameshatambua rangi huwa hawana subra kwa chochote kitakachokuja karibu
nao.na hasa watoto wenye umri wa mwaka mmoja
hadi miwili.
Wao wakikosa cha
kushika katika uso wako basi watakufinya ama kukukodoa jicho! Kama unamiwani
mtaigombea!! Kama una kofia wao ni halali yao ama kama mama ana manywele basi
yatavutwa weee, nawe baba kama una ndevu utapata habari yao!
Bado sijaelewa ni kwanini
vitu vya juu ya shingo huwavutia sana watoto, maana wakati mwingine vitu hivyo
havina mvuto, maana watoto na rangi na mwao. Wanasaikolojia mnahusika hapa
katika kunielimisha name niko tayari!
Baba mtakatifu Francis
,ambaye ni pope wa kwanza kutoka South
America,amechaguliwa kua MAN OF THE YEAR
2013! Kuna matukio mengi sana yasiyotarajiwa kufanywa na pope katika ziara zake
yeye hua ana vunja mwiko, na kuruhusu hata watoto wadogo wamchezee, wamshike
watakavyo na yeye kutetea kua waachwe wafanye wafanyacho!na hata watu wenye
taswira za kuogofya yeye husogea karibu nao na kuwabusu ama kuwakumbata! What a
pope! Kwa upande mwingine BWANA YESU
ALISEMA WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU! Labda kutoka na usemi huo ndo
yanatokea tuyaonayo,lakini kwa upande mwingine kwa wasio na mapenzi mema na
kiongozi huyo wanaweza kumtumia mtoto kufanya walichodhamiria! Ni mtazamo tu
huu!
Mtazame pope na mtoto
huyu aliyeamua kuvutiwa na kichwa cha pope na kofia yake.
Kofia ya Pope
ikiondolewa pahala pake.
Aha baada ya kuondoa kofia kumbe dogo alivutiwa na nywele za Pope Francisiiii! sasa zinakaguliwa kwa umakini mkubwa!
Well, yatosha sasa dogooo! ah wapi Pope anajitahidi kurejesha kikofia na dogo akwa bado haja kidhi haja yake ya ukaguzi.YES HE'S THE MAN OF THE YEAR
No comments:
Post a Comment