Shangwe na hoi hoi za mashabiki wa mchezo wa
American football katika mji wa Seattle nchini Marekani zilisababisha kishindo kikubwa
cha makelele kusababisha tetemeko dogo la ardhi,kwa mujibu wa wanasayansi.
Mashabiki waliokuwa waliokuwa na furaha
waliruka huku na huko lilipofungwa bao la mapema katika mchezo kati ya Seattle
Seahawks na New Orleans Saints.
Kituo kinachochunguza na kupima mitetemeko ya
ardhi The Pacific Northwest Seismic Network kilibaini mtikisiko wa vipimo baina
ya 1 na 2 ya nguvu za tetemeko la ardhi.Seahawks walishinda mchezo huo katika uwanja
wa CenturyLink Field kwa pointi 34-7.
Mkurugenzi wa kituo cha Pacific Northwest
Seismic Network John Vidale aliiambia CNN kwamba wanasayansi wake walirikodi
mitikisiko 5 tofauti ya ardhi wakati wa mchezo huo.
Hii si mara ya kwanza; kwani mwaka 2011
mashabiki wanaoshangilia walisababisha ardhi ya Seattle kutikisika katika
mchezo mwingine wa American Football.
Uwanja wa CenturyLink Field, ambao ni wazi pia
uliweka rekodi ya dunia ya takwimu za Guinness World Record
No comments:
Post a Comment