LIGI KUU YA ENGLAND ILIENDELEA TENA WIKIENDI HII IKISHUHUDIA
TIMU ZOTE KUMI ZIKIWA VIWANJANI KUSAKA POINTI TATU MUHIMU .
VINARA WA LIGI HIYO WASHIKA BUNDUKI WA ARSENAL WALIWAFUNGA
CARDIFF CITY KWA MABAO MATATU BILA KATIKA MCHEZO ULIOPIGWA SIKU YA JUMAMOSI .
KATIKA MCHEZO HUO MABAO YA ARSENAL YALIFUNGWA NA AARON RAMSAY
AMBAYE ALIFUNGA MABAO MAWILI NA MATHIEU FLAMINI.
TOTTENHAM HOTSPURS NA
MANCHESTER UNITED WALITOKA SARE YA MABAO MAWILI KWA MAWILI KATIKA MCHEZO
ULIOPIGWA KWENYE UWANJA WA WHITE HART LANE .
MABAO YA SPURS YALIFUNGWA NA KYLE WALKER NA ALEX SANDRO HUKU
WAYNE ROONEY AKIFUNGA MABAO YOTE MAWILI YA MAN UNITED .
CHELSEA WAKIWA KWENYE UWANJA WAO WA STAMFORD BRIDGE WALIWAFUNGA
SOUTHAMPTON MABAO MATATU KWA MOJA . MABAO YA CHELSEA YALIFUNGWA NA GARY KEIHIL
, JOHN TERRY NA DEMBA BA HUKU JAY RODRIGUEZ AKIFUNGA BAO PEKEE LA SOUTHAMPTON.
MANCHESTER CITY NAO WALIENDELEZA REKODI YAO YA KUFANYA VIZURI
WANAPOCHEZA MECHI ZA NYUMBANI NA SAFARI HII WALIWAFUNGA SWANSEA CITY MABAO
MATATU BILA . WAFUNGAJI WA CITY KWENYE MCHEZO HUO WALIKUWA SAMIR NASRI AMBAYE
ALIFUNGA MABAO MAWILI NA ALVARO NEGREDO.
LIVERPOOL AMBAO JANA WALIKUWA WANACHEZA BILA NYOTA WAO DANIEL
STARIJ WALIPOTEZA MCHEZO WAO MBELE YA HULL CITY KWA MABAO MATATU KWA MOJA .
MABAO YA HULL YALIFUNGWA NA
JEK LIVAMO,DAVID MEYLER NA BEKI WA LIVERPOOL MARTIN SKATOL ALIYEJIFUNGA
MWENYEWE HUKU LIVERPOOL WAKIPATA BAO LAO PEKEE KUPITIA KWA STEVEN GERRARD.
NCHINI HISPANIA ATLETICO MADRID WALIWAFUNGA ELCHE KWA MABAO
MAWILI BILA KATIKA MCHEZO ULIOPIGWA SIKU YA JUMAMOSI .
MABAO YA ATLETICO
YALIFUNGWA NA DIEGO COSTA PAMOJA NA KOKE
.
KATIKA MCHEZO MWINGINE REAL MADRID WALIENDELEA KUZINYANYASA TIMU
ZINAZOKUJA MBELE YAO BAADA YA KUWAFUNGA VAYADOLID KWA MABAO MANNE BILA .
MABAO MATATU YALIFUNGWA
NA MCHEZAJI GHALI KULIKO WOTE DUNIANI GARETH BEIL HUKU KARIM BENZEMA AKIFUNGA
BAO MOJA .
KATIKA MCHEZO HUU WACHEZAJI WA REAL MADRID WALIVUNJA REKODI YAO
WENYEWE KWA KUPIGA PASI 745 .
SIKU YA JUMAPILI MABINGWA WATETEZI WA LIGI HII YA HISPANIA
PRIMERA LIGA FC BARCELONA WALIJIKUTA WAKIPOTEZA MCHEZO WA PILI MFULULIZO BAADA
YA KUKUBALI KIPIGO CHA BAO MOJA BILA MBELE YA ATHLETIC BILBAO .
GOLI LILILOPELEKA MSIBA KWA BARCELONA LILIFUNGWA NA IKER MUNIAN.
NCHINI UJERUMANI MABINGWA WATETEZI WA BUNDESLIGA BAYAN MUNICH
WALIENDELEZA UBABE WAO SFAARI WAKIWAFUNGA BRONSHWEIG MABAO MAWILI BILA .
MABAO YOTE MAWILI YALIFUNGWA NA ARJEN ROBBEN .
NAO BORRUSIA DORTMUND WALIWAFUNGA MAINZ MABAO MATATU KWA MOJA .
KATIKA MCHEZO HUO
DORTMUND WALIFUNGA KUPITIA KWA PIERRE EMERICK OBAMEYANG NA ROBERT LEVANDOSKI AMBAYE ALIFUNGA MABAO
MAWILI.
NCHINI ITALIA JUVENTUS WALIREJEA KWENYE KILELE CHA LIGI YA SERIE
A KWA KUWAFUNGA UDINESE BAO MOJA BILA .
BAO HILO LA NGAMA LILIFUNGWA NA MHISPANIA FERNANDO YORENTE .
AS ROMA WALIENDELEA NA HARAKATI ZAO ZA KUSAKA REKODI MPYA YA
KUTOKA SARE KWENYE MECHI NYINGI BAADA YA KUWEKA ILE YA KUSHINDA MECHI KUMI
MFULULIZO .
ROMA NA ATALANTA BERGAMO WALITOKA SARE YA BAO MOJA KWA MOJA
IKIWA SARE YA NNE MFULULIZO KWA ROMA .
ATALANTA NDIO WALIOANZA KUFUNGA KUPITIA KWA DAVIDE BRIVIO KABLA
YA KEVIN STRUTMAN HAJAISAWAZISHIA ROMA .
NCHINI UFARANSA MABINGWA WATETEZI PARIS SAINT GERMAIN
WALIWAFUNGA MABINGWA WA ZAMANI OLYMPIQUE LYON KWA MABAO MANNE BILA .
WAFUNGAJI WA PSG WALIKUWA ZLATAN IBRAHIMOVIC AMBAYE ALIFUNGA
MABAO MAWILI , EDINSON CAVANNI NA THIAGO SILVA .
SIKU YA JUMAMOSI AS MONACO WALIWAFUNGA RENNES MABAO MAWILI BILA
. WAFUNGAJI KWENYE MCHEZO HUO WALIKUWA JAMES RODRIGUEZ NA ANTHONY MARTIAL .
NAO LILLE METROPOLE WALIWAFUNGA VALENSION KWA BAO MOJA BILA .
BAO HILO PEKEE LILIFUNGWA NA RONNY .
No comments:
Post a Comment