Kocha Ernie Brandts
ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa
Yanga, Ernie Brandts amesema kiasi fulani hafurahii na inamchanganya kuona
amefukuzwa kazi na anaendelea kubaki nchini.
Akizungumza jijini Dar
es Salaam, Brandts amesema inamuwia vigumu kuona anaendelea kubaki jijini Dar
es Salaam.
“Wangeweza kunipa
malipo yangu ili niende mapema. Wachezaji wanajua mimi nimefukuzwa Yanga,
lakini vipi leo naendelea kufanya nao kazi.
“Ningependa nimalizane
vizuri na uongozi wa Yanga na Wanayanga wote ili niondoke kwa amani na si
mizozo,” alisema.
Kocha huyo raia wa
Uholanzi ametupiwa virago vyake mara baada ya timu yake kufungwa kwa mabao 3-1
na watani wao Simba katika mechi ya kirafiki ya Nani Mtani Jembe.
No comments:
Post a Comment