Askari
akilinda mali ilopinduka.
Waokozi wana wasiwasi
kuwa pengine watu kadha wamenasa chini ya treni iliyopinduka katika mitaa ya
Kibera, Nairobi - eneo la watu maskini.
Watu kama kumi
walijeruhiwa wakati mabehewa mane ya mizigo yalipopinduka juu ya vibanda kando
ya njia ya reli.
Waokozi wanajaribu
kutafuta nafasi katika mtaa wenye nyumba zilizogandana sana, ili kuleta mashini
ya kunyanyua mabehewa ili kuwafikia wale walionasa.
Mabehewa yalianguka juu
ya vibanda vilivyo karibu na njia ya reli.
Magazeti yanaarifu kuwa
kazi za uokozi zimezingika kwa sababu watu wengi wamezonga eneo hilo.
No comments:
Post a Comment