Tuesday, December 24, 2013

WAZIRI WA UCHUKUZI, DK. HARRISON MWAKYEMBE AFUNGA MWAKA KWA KUWATAMBULISHA RASMI KATIBU MKUU NA NAIBU KATIBU MKUU KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM



Sehemu ya Watendaji wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Shaaban Mwinjaka(Hayupo pichani) wakati wa mkutano maalum wa kufunga mwaka na kuwatambulisha rasmi viongozi hao uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na wafanyakazi wa Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo leo jioni katika mkutano maalum wa kufunga mwaka na kuwakaribisha rasmi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(kulia kwa Waziri Mwakyembe)na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange(kushoto kwa Waziri Mwakyembe Katika ukumbi wa Karimjee,jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs Monica Mwamunyange akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kufunga mwaka na kuwakaribisha rasmi Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu huyo. Mkutano huo umefanyika leo jioni katika ukumbi Karimjee jijjini Dar es Salaam. Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo amesisitiza ushirikiano na kujiwekea malengo katika utendaji kazi wa kila siku.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(wa kwanza kulia mstari wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange(wa pili kutoka kushoto mstari wa kwanza) na wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Uchukuzi leo jioni katika Mkutano maalum wa Waziri wa Uchukuzi kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Wafanyakazi wa WIzara hiyo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(wa tatu kutoka kulia mstario wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange (wa pili kutoka kushoto mstari wa kwanza) na baadhi ya watumishi wa  Wizara ya Uchukuzi leo jioni katika Mkutano maalum wa Waziri wa Uchukuzi kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Wafanyakazi wa Wizara hiyo.

No comments:

Post a Comment