Tuesday, December 10, 2013

WATANZANIA WAASWA KUHESHIMU HAKI ZA MTOTO

DSC_0960
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB), Jaji Mstaafu Amir Manento akizungumza na waandishi wa habari wakati mdahalo wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ambayo hufanyika tarehe 10 mwezi Disemba kila mwaka.

.Jaji Manento asema ni uvunjifu wa sheria kwenda na watoto harusini
Na Damas Makangale, MOblog
WAZAZI na Walezi wameaswa kuacha mara moja tabia ya kwenda na watoto katika sherehe na harusi mbalimbali za kwa sababu ni kosa la Jinai kwa mujibu wa sheria na Haki za Mtoto. MOblog inaripoti.
Akizungumza kwenye mdahalo wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ambao huadhimisha kila tarehe 10 mwezi Disemba kila mwaka, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania, Jaji Mstaafu Amir Manento amesema kwa mujibu wa sheria na Haki za Mtoto wazazi au walezi hawaruhusi kwenda na watoto katika sherehe za usiku.
“wazazi na walezi na watu wa kawaida wanamazoea ya kwenda na watoto kwenye sherehe za harusi na majumba ya starehe lakini kwa mujibu wa sheria na haki za mtoto na marekebisho yake ya 2009 ni uvunjifu wa sheria na haki za mtoto,” amesema Jaji Manento.
DSC_0885
Meza Kuu kati kati ni msimamizi (moderator) Dkt Khoti Kamanga toka UDSM, kushoto kwake ni Bw, Godfrey Mulisa toka UN, kushoto mwisho ni Mwakilishi Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Bw, Harold Sungusia na kulia kwa msimamizi ni Francis Nzuki kutoka Tume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala Bora na mwisho kulia ni Bi, Felistas Mushi toka Wizara ya Sheria na Katiba.
Amesema kuwa Tanzania iliridhia tamko rasmi la Haki za Binadamu ili pamoja na mambo mengine kulinda Uhuru na Haki za Binadamu pamoja na haki ya kuishi.
“Tarehe 10 Disemba imeainishwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu. Kuainishwa siku ya Kimataifa ya Haki za binadamu kunakumbusha juhudi kubwa zilizofanywa kwa lengo la kuwafanya watu waheshimu Haki za Binadamu kote duniani,” alisisitiza.
Jaji Manento amesema suala la kuheshimiwa haki za binadamu lilipewa kipaumbele cha kwanza wakati wawakilishi wa nchi mbalimbali walipokuwa wakibuni Hati ya Umoja wa Mataifa.
Aliongeza kuwa Januari mwaka 1947 iliundwa kamati ya haki za binadamu na hati ya kamisheni hiyo ilipasishwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Disemba 1948.
Jaji manento amesema kuwa kwa msingi huo siku hiyo ya tarehe 10 Disemba ilitambuliwa kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu duniani kote.
DSC_0930
Mwakilishi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bw. Harold Sungusia akiwasilisha mada yake kuhusu historia na chimbuko la Haki za Binadamu katika bara la Afrika tangu enzi za miaka 1200 kwenye nchi ya Mali (Mali Empire).
Amesema kuwa imepita zaidi ya miongo sita sasa tangu kutolewa Azimio la Haki za Binadamu ambalo linakusanya thamani za pamoja kwa ajili ya kuondoa ubaguzi, kueneza uhuru na kupambana na dhuluma dhidi ya binadamu duniani.
Alilisitiza kwamba hapana shaka kuwa kutetea haki za binadamu kwa ajili ya kutimiza lengo hilo ni kazi yenye thamani kubwa. Hata hivyo aliongeza kadhia hiyo inayumbishwa na nchi za Magharibi ambazo zinatumia haki za binadamu na ripoti zinazotolewa na taasisi za haki za binadamu kama nyenzo na fimbo ya kisiasa kwa baadhi ya nchi zinazoendelea.
Kauli mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ni “mafanikio na changamoto katika kuhamasisha na kulinda Haki za Binadamu Tanzania” .
DSC_1003
Juu na chini ni Baadhi ya vijana wa shule za sekondari mbalimbali na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
DSC_0972
Mjumbe kutoka Tume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala bora Bw, Francis Nzuki (wa pili kulia) akizungumzia uzoefu wake katika kuhamasisha Haki za binadamu katika Magereza nchini Tanzania hasa kwa Wafungwa.
DSC_0989
Mwakilishi kutoka Wizara ya Sheria na Katiba, Bi.Felistas Mushi akiwasilisha mada kuhusu kwanini kuna mpango mkakati wa serikali katika kutekeleza Haki za Binadamu nchini Tanzania.
DSC_1052
Mtaalamu wa mambo ya Utawala bora , Grainne Kilcullen kutoka UNDP akiwahamasisha vijana waliohudhuria mdahalo huo kuwa mstari wa mbele katika kusimamia Haki za Binadamu na kuwaelimisha jamii inayowazunguka kuzitambua Haki zao za msingi.
DSC_1061
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania, Jaji Mstaafu Amir Manento (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za sheria wa Tume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala bora, Bw. Nabor Assey ( wa pili lulia), Mtaalamu wa mambo ya Utawala bora , Grainne Kilcullen kutoka UNDP na Afisa Habari wa Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumziwa kwenye mdahalo huo.
DSC_1025
Pichani Juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakitoa maoni na kuchangia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mdahalo huo.
DSC_1029
DSC_1043
Wanafunzi mbalimbali wakipata maelezo kutoka kwa Investigation Officer wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Getrude Alex (kushoto) juu ya machapisho mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini.
DSC_1067
Afisa Habari wa Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama akitoa neno la shukrani kwa wote walioshiriki mdahalo huo.

No comments:

Post a Comment