Baadhi
ya wakazi wa mjini Singida, wakiwa wamekusanyika katika duka la wakala wa
M-pesa lililopo kwenye taasisi ya elimu ya watu wazima, muda mfupi baada ya
mmiliki wa duka hilo Mashaka Omari Makiya,kujipiga risasi kwa kutumia Bastola
yake na kusababisha kifo chake.
Mwandishi
wa habari wa radio na TV Clouds mkoani Singida, John,akisoma wosia (haupo
kwenye picha) ulioachwa na mfanyabiashara
Mashaka Omari Makiya,aliyejiua kwa kujipiga risasi kwa bastola yake.Wosia huo
umedai kuwa wadogo wa marehemu wakabidhiwe nyumba na fedha alizoziacha.
WAKALA
Maarufa wa M-pesa Vodacom na Mkazi wa Kibaoni mjini Singida Mashaka Omari
Makiya (30) amejipiga risasi kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo.Mashaka
maarufu kwa jina la Mashakom, amejipiga risasi kwa kutumia bastola yake aina ya
‘silencer’ usiku wa Desemba 27 mwaka huu, nyumbani kwake Ipembe mjini hapa.
Shuhuda
wa tukio hilo,Shija John amesema Desemba 28 mwaka huu saa saba mchana askari
polisi walifika nyumbani kwa marehemu iliyopo mkabala na nyumba ya kulala
wageni ya Meatu eneo la Ipembe.Amesema askari polisi hao waliingia chumbani kwa
Mashaka ambapo walikuta mwili wa mfanyabiashara huyo ukiwa sakafuni.Pia
walikuta bastola yake ikiwa pembeni mwa mwili huo pamoja na simu zake tatu.
“Taarifa
nilizonazo ni kwamba mfanyakazi wa Mashaka aligundua tukio hilo na kisha alitoa
taarifa kituo kikuu cha kati cha polisi na askari walifika mara moja”,amesema.Katika
hatua nyingine, mwandishi wa habari hizi aliweza kufika kwenye moja ya maduka
yake matatu ya M-pesa na kushuhudia ujumbe wa maandishi ulioachwa na Mashaka
ndani ya gari lake jeusi.
Pamoja
na askari polisi kukataa kutoa kibali kwa waandishi habari kusoma ujumbe huo au kuupiga picha,watu
waliobahatika kuusoma ukiwa ndani ya gari wamedai kuwa marehemu amemhusisha na
kifo chake mfanyabiashara mmoja (jina tunalo) aliyekuwa na mahusiano ya karibu
ya kibiashara pia marehemu Mashaka ameagiza kuwa nyumba na fedha zake wapewe
wadogo zake.
Kifo
cha Mashaka kimezua hofu kubwa na kazi ya uwakala wa M-pesa kwa madai kwamba
katika miaka michache waliokuwa wafanyabiasha wa uwakala huo,Tembs na Rweyemamu
wote wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida,
SACP Geofrey Kamwela amesema bado hajapata taarifa hizo na ameahidi
kulifuatilia na kutoa habari ili jamii iweze kujua kilichojiri
No comments:
Post a Comment