Wachezaji
wa Tottenham
Tottenham imeandika
ushindi wake wa pili mfululizi katika uwanja wa Old Trafford dhidi ya wenyeji
Manchester United na kujizolea alama tatu muhimu na kupanda hadi nafasi ya sita
kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier.
Mabingwa hao watetezi,
walianza vyema lakini Emmanuel Adebayor, alijikakamua na kuifungia Tottenham
bao lake la kwanza kwa kichwa baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Christian
Eriksen.
Eriksen naye akaongeza
la pili baada ya kuchapa mkwaju mkali uliomuacha kipa wa Manchester United
kinywa wazi.
Lakini katika kipindi
cha pili Danny Welbeck akafufua matumaini ya United kwa kuifungia United bao
moja na kufanya mambo kuwa Tottenham mawili United Moja.
Baada ya bao hilo la
Welbeck United ilifanya mashambulio kadhaa katika lango la Tottenham lakini juhudi
zao ziligongwa mwamba.
Wachezaji wa Man United
baada ya kushindwa na Tottenham
Javier Hernandez nusura
asawazishe dakika za mwisho mwisho lakini mkwaju wake ukaokolewa.
Matokeo hayo yalikuwa
mazuri kwa kocha mpya wa Tottenham Tim Sherwood, ambaye hajashindwa katika
mechi nne alizosimamia.
Kabla ya ushindi wao wa
magoli matatu kwa mawili katika uwanja huo mwaka uliopita, Tottenham ilikuwa
haijawahi kuishinda United katika uwanja wa Old Trafford kwa zaidi ya miaka 23.
Manchester United sasa
inashikilia nafasi ya saba alama kumi na moja nyuma ya vinara wa ligi hiyo kwa
sasa Arsenal iliyo na alama 45.
Manchester City ni ya
pili alama moja nyuma ya Arsenal huku Chelsea ikiwa ya tatu na alama 43.
No comments:
Post a Comment