Pamoja
na Cristiano Ronaldo kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia lakini raisi wa
Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesisitiza kwamba kamwe hawawezi
kumbadilisha winga wao
Franck
Ribery na kumchukua mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo. Winga wa
Ufaransa Ribery alishika nafasi ya tatu nyuma ya mshambuliaji wa Real Madrid na
Lionel Messi katika kura za Ballon d'or. Rummenigge anasema
hajasangazwa
kwamba Ronaldo ameshinda tuzo hiyo lakini bado akasisitiza kwamba Ribery ana thamani
kubwa kwao kuliko Ronaldo. "Mara tu ulipoona kikundi cha watu
waliomsindikiza Ronaldo kuja kwenye tuzo kutoka Madrid,
haukuhitaji
kuwa mtume kujua nini kinafuatia," mchezaji huyo wa zamani wa Ujerumani yaMagharibi
aliiambia Bild.
"Lakini
Bayern Munich hatuwezi kumbadilisha Frank na Ronaldo." Rummenigge pia
akasema kwamba Mabavaria watafanya kila waliwezalo kuhakikisha wanaendelea kuwa
na Mario Mandzukic na Arjen Robben.
No comments:
Post a Comment