Bingwa wa zamani katika
soka ya Ureno, Eusebio da Silva
Ferreira, amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 71. Chui Mweusi, kama
ulivyokuwa umaarufu wake, alizaliwa nchini Msumbiji na akawa maarufu nchini
Ureno, ambako anatambuliwa kama shujaa wa soka.
Katika miaka ya '60
alionekana kama mchezaji pekee bingwa nchini humo kutokana na nguvu zake za
kiriadha na uwezo wa kufunga vyema magoli. Aliipatia ushindi timu yake ya taifa
ya Ureno katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1966.
Kocha wa Chelsea ya
Uingereza, Jose Mourinho, ambaye naye ni Mreno, amemtaja Euebio kama mchezaji
wa milele, ambapo mchezaji nyota wa Real Madrid ya Hispania na nahodha wa timu
ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amesema Eusebio ni shujaa wa siku
zote.
Eusebio ameacha mke
anayeitwa Flora, binti wawili, na wajukuu kadhaa
No comments:
Post a Comment