Bingwa zamani wa uzito wa juu duniani Mike Tyson amepigwa
marufuku kuingia nchini Uingereza kuzindua kitabu chake. Hatua hiyo inatokana
na mabadiko katika sheria za uhamiaji.
Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba bondia
huyo wa Marekani ambaye aliwahi kuhukumiwa kwa ubakaji akitazamiwa kuwasili
nchini humo wiki hii akitokea paris-Ufaransa, kwa uzinduzi wa kitabu cha maisha
yake, kiitwacho “ ukweli usipingika.” Sheria mpya za uhamiaji hata hivyo
zinaeleza kwamba mtu yeyote aliyewahi kupatikana na hatia na kutumikia kifungo
cha zaidi ya miaka mine jela hatoruhusiwa kuingia Uingereza .
Tyson mwenye umri wa miaka 47 alihukumiwa kifungo cha
miaka sita mwaka 1992 kwa kumbaka mrembo mmoja wa zamani. Mchapishaji wa kitabu
chake harper Collins alikaririwa akisema kulikuwa na mabadiliko katika sheria
za uhamiaji uza Uingereza Desemba mwaka jana 2012 ambazo hawakuzijuwa na
kutokana na hayo walilazimika kubadili ratiba na badala yake kitabu hicho
kuzinduliwa eneo moja la jiji la Paris.
Tyson alikuwa bingwa wa kwanza wa dunia mwenye umri mdogo
1986 alipokuwa na miaka 20 na bondia wa kwanza kushikilia mataji matatu makubwa
ya ubingwa wa ndondi duniani kwa wakati mmoja mwaka mmoja baadae. Mwaka 2000
Tyson alipigana nchini Uingereza dhidi ya Julius Francis mjini Manchester na
baadae mwaka huo huo akachuana baadaye na Lou Savarese mjini Glasgow.
No comments:
Post a Comment