Wednesday, January 8, 2014

SAFARI YA BONGE NA MIAKA 14 YA CLOUDS FM YAFANA JIJINI MWANZA.

Pichani Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (mtu wa watu) Mhe. Stanslaus Mabula (katikati) akiwa na Afisa Habari wa Jiji la Mwanza Joseph Mlinzi (kushoto) wakifurahia jambo na Bonge wa Power Breakfast huku wakiwa T-Shirt za 88.1 Clouds Fm Mwanza. 
Bonge wa PB akipata flash ya pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula (wa pili toka kushoto) Afisa Habari wa Jiji hilo Joseph Mlinzi (wa kwanza kushoto )  pamoja na Mwekezaji wa Mwanza toka Ndege Insurance iliyosambaa kote nchini sasa Dr. Sebastian Ndege (Jembe).
"Jembe we tayari ni Mwanamwanza tu kubali kataa...na ukibisha naandamana" says Bonge (L) to Dr. Sebastian Ndege (R).
Bonge akikabidhi mzigo kwa Pilly Mgori ambaye ni Mkuu wa masoko Clouds Media Mwanza
Bonge alimng'arisha pia mwanahabari Peter Fabian, anaye andikia gazeti la Mtanzania na  moja kati ya magazeti ya ndani mkoani Mwanza linalojulikana kama Mzawa.
Bonge na Mwenyekiti wa Mwanza Kwanza ambaye pia ni mtangazaji wa redio rafiki Passion Fm Mwanza, Philbert Kabago 
Safari ya Bonge kushow love na miaka 14 ya Clouds Media ilijikita Pasiansi kwa madereva wa bodaboda.
Unamjua mdogo wake na PNC? Basi zingatia picha hii kwa makiiiiiini utang'amua.....!!
"Lazima tung'ae"
"88.1 Ni masafa ya burudani pande hizi, now ni tyme ya kurejea town. huku tukisikiliza redio ya watu Clouds 14"
Dreva tax Victor Magambo (kulia) akikamata yake.
Mpiga picha maarufu wa jijini Mwanza aliyeweka kambi katika kipitashoto cha kitalii cha  Samaki aliyesikika kupitia Jahazi la Clouds Fm Joseph Pima naye alihusika na shangwe za Clouds 14.
Madreva taxi kituo cha Tanesco zamani.
Mara nkabaaaaaa....!!! Bonge akawakakamatisha mihuri ya 88.1.
Yebo yes... ni Albert G. Sengo (L) na Bonge (R).
88.1 ilihusishwa pia pande za 'reception' at Gold Crest Mwanza...
Hadi mida ya Night kali na  mmoja kati ya wadau nambari moko wa Clouds Fm Mr. Mgulu.

No comments:

Post a Comment