BONDIA bora wa mwaka
2013,2014 katika uzito wa KG 63 Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ (pichani)
amesaini mkataba wa kupambana na Cosmas Cheka Februari 8 mwaka huu katika
ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.
Mara baada ya kusaini
mkataba huo wa kucheza raundi 10 za ubingwa wa Taifa Kg 60 amesema atafanya
mazoezi ya kutosha kuhakikisha ana msambaratisha mpinzani wake raundi za awali
kwa kuwa alikuwa anachonga sana juu yake.
Mpambano huo
unaodhaminiwa na Promota Maarufu nchini Jay Msangi utakuwa na msisimko wa aina
yake kutokana na mabondia hawo kuwa gumzo katika ulimwengu wa masumbwi ndani na
nje ya nchi.
King Class aliongeza
kwa kusema;”Nipo fiti, nimejiandaa na ninasubiri tu kuvishwa ubingwa huo wa
Taifa kwani Cheka hana ujanja kwangu mbinu zake zote nimesha zikamata”.
King Class Mawe
ananolewa na jopo la makocha wanao ongozwa na Habibu Kinyogoli ‘Masta’ Rajabu
Mhamila ‘Super D’ na Kondo Nasoro.
Bondio huyo
amewashukuru wadau wa mchezo wa ngumi kwa kumuwezesha kuchaguliwa kuwa bondia
bora wa mwaka katika uzito wake na kuwapita mabondia wengine wanne na yeye
kuibuka kidedea katika kin’yan’gan’yiro hicho
No comments:
Post a Comment